25.8 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

Mabasi 36 ya safari za usiku yasitishiwa leseni

Na Esther Mnyika Mtanzania Digital

Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) imesitisha leseni kwa mabasi 36 yaliyokuwa yakifanya safari za usiku kutokana na kuchezea mfumo wa kufuatilia mwenendo wa magari VTC.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Novemba 9,2023 Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu LATRA, CPA Habibu Suluo wakati akitoa tathimini ya safari za mabasi kwa saa 24 kuanzia Oktoba 5 hadi Novemba 6,2023 amesema pamoja na mabasi wamefungia pia madereva 10 walochezea mfumo.

Pia madereva 666 wameandika faini kwa makosa ya mwendokasi na 32 wakifikishwa mahakamani, huku 50 wakipewa onyo.

Amesema Novemba 6, 2023, LATRA ilitoa ratiba za usiku kwa mabasi 246 kwa kampuni za usafirishaji 46 kwa jumla ya njia 26 zinazoanzia Jijini Dar es salaam.

“Kampuni zilizoongoza kuchezea mfumo wa VTS na mwendokasi ni pamoja capricorn, ambapo jumla ya mabasi tisa yalifungiwa, Abood wawili, Dar express mawili, huku kampuni 23 za mabasi zikifugiwa basi mojamoja,” amesema CPA Suluo

CPA Suluo amesema katika kufatilia mwenendo wa utoaji huduma kwa kutumia nyenzo mbalimbali zikiwemo mfumo wa VTS, ratiba za mabasi, ukaguzi wa maeneo mbalimbali ilibaini baadhi ya wasafirishaji kuchezea mfumo wa VTS na kwenda mwendokasi unaotakiwa kisheria zaidi ikiwemo taarifa za abiria kutokuzingatiwa ipasavyo .

“Mabasi 197 sawa na asilimia 80 yanaenda mwendokasi kati ya kilometa 86-89 kwa saa, wanaendesha mwendokasi kati ya kilometa 90 _103 kwa saa,”amesema.

Amesema kuwa katika kuendana na azma ya serikali ya kuruhusu utoaji huduma saa 24 ni kwa mujibu ya sheria ya LATRA sura ya 413 na Sheria ya usalama barabarani sura 168 kifungu 23 na kifungu 28 (6) madereva waliofugiwa hawataruhisiwa kuendesha gari lolote kwa kipindi chote cha kutumikia adhabu zao.

“Ili dereva aweze kurejea atalazimika kuzingatia matakwa ya sheria ya usalama barabarani sura ya 168 kifungu cha 23 na kifungu 28 (6),”amesisitiza

Aidha amesema baada ya kutumikia adhabu hiyo dereva atatakiwa kuomba kufunguliwa atalazimika kutahiniwa ili kupima uwezo wake katika taaluma yake.

Naye Kamanda wa Polisi Kikosi Cha Usalama Barabarani SACP Ramadhani Ng’anzi amesema madereva ambao watakuwa wakienda kinyume watafugiwa ikiwemo kufikishwa mahakamani na kufutiwa leseni.

Amesema madereva hao 10 wamefugiwa kati mwezi mmoja hadi sita kutokana na kuchezea mfumo wa VTS jambo ambalo ni hatari linaweza kusababisha ajali.

“Dereva yoyote anayechezea mfumo wa VTS na tukagundua ana sifa, kifaa chochote anachofaa kuendesha ni Power Tira na sio gari ya abiria ,”amesema.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Chama Cha Wamiliki Mabasi Tanzania (TABOA), Priscus Joseph, amewaomba madereva kutokwenda mwendokasi kwa lengo la kuwahi.

“Nitoe rai kwa madereva kupunguza mwendo hasa katika kipindi hiki kutokana na kuwepo kwa mvua nyinyi nawaomba tupuguze mwendokasi,”amesisitiza Joseph

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles