25.4 C
Dar es Salaam
Monday, November 11, 2024

Contact us: [email protected]

Wakazi Msomera wamshukuru Rais Samia

*Awapa Hatimiliki za Ardhi
*Awapa ekari 2.5 za makazi na 5 za mashamba kila mmoja
*Wataka kauli za wanasiasa zipuuzwe

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Wakazi wa Msomera Wilayani Handeni mkoa wa Tanga waliohama kwa hiari kutoka Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro wamemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kwa kuwawezesha kupata hatimiliki za ardhi za maeneo yao waliyopewa na Serikali.

Shukrani hizo zimetolewa na wakazi hao wakati wakipokea hatimiliki za ardhi katika mkutano wao na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Geophrey Pinda katika Kijiji cha Msomera.

Wakazi hao ambao waliohamia kwa hiari na wale ambao ni wenyeji wa Msomera wametaka kupuuzwa kwa kauli za wanasiasa wanaobeza mpango huo kwani umekuwa ni neema kwao na vizazi vyao kwa kupata makazi ya kudumu yaliyo na hatimiliki kitu ambacho kilikuwa ni ndoto kwa jamii ya kifugaji.

Kwa mujibu wa Kamishna wa Ardhi Msaidizi mkoa wa Tanga, Tumaini Gwakisa amesema hadi sasa hati zilizotolewa kwa wakazi hao ni 1,142.

Aidha, eneo lililopangwa na kupimwa kwa matumizi ya mashamba na viwanja lina jumla ya viwanja na mashamba 4,509.

Hii imezingatia maelekezo ya Serikali ya kuwa na maeneo ya ukubwa wa viwanja vya ekari 2.5 kwa matumizi ya makazi na maeneo ya ukubwa wa ekari 5 kwa matumizi ya Mashamba ambazo kila mkazi atayehamia kwa hiari katika eneo hilo atapewa na Serikali pamoja na nyaraka ya umiliki wake.

Aidha, eneo la malisho lenye ukubwa wa hekta 22,000 limepangwa na kupimwa kwa ajili ya mifugo kwa wananchi hao wa jamii ya kifugaji wanaohamia kwa hiari kutoka Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro mkoani Arusha.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles