25.5 C
Dar es Salaam
Tuesday, December 17, 2024

Contact us: [email protected]

Washindi 100 wa Mtoko wa Kibingwa na Betika kushuhudia Derby ya Kariakoo

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital 

WASHINDI 100 wa Kampeni ya Mtoko wa Kibingwa kupitia kampuni ya Betika wamewasili rasmi jijini Dar es Salaam kushuhudia derby ya Kariakoo kesho Aprili 16, 2023 itakayopigwa katika dimba la Benjamini Mkapa.

Ikumbukwe kuwa mpambano huo wa mzunguko wa pili kwenye ligi unazikutanisha Simba ambaye ndiye timu mwenyeji dhihdi ya Yanga.

Akizungumza na Waandishi wa Habari mapema leo Aprili 15, kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julias Nyerere wakati wa mapokezi ya washindi hao, Afisa Uhusiano wa Kampuni ya Betika, Nelson Pius amesema kuwasili kwa washindi hao kunaleta historia ndani ya msimu huo wa 5 kutimiza washindi 100 kutoka mikoa mbalimbali huku mshindi mmoja akiwa Mwanamke kutoka Chamazi jijini Dar es Salaam.

“Tayari washindi wetu wamewasili kutoka mikoani ikiwemo Geita, Mtwara, Rukwa, Simiyu, Songwe, Dar es Salaam na sehemu mbalimbali ni furaha yetu kuwa watakwenda kutazama derby ya Kariakoo kama dhamira ya kampuni ya betika ilivyoandaa shughuli hii tangu kuzinduliwa kwa kampeni awali Febuari, mwaka huu,” amesema Pius.

Pius ameeleza kuwa washindi hao wamepatikana kupitia droo za kila siku ambapo mshiriki aliweza kuweka ubashiri wake kwa dau la Sh 500.

“Tayari washindi wetu wametuwa dar mapema hivyo kutafatiwa na bata la mtoko wa kibingwa itakayofanyika kidimbwi huku siku ya kesho watasindikizwa na king’ora hadi uwanjani na watapata huduma ya kipekee,” ameongeza.

Kwa upande wake mshindi kutoka mkoani Simiyu, Bahame Balele amesema amefurahi kufika Dar es Salaam kwa usafiri wa mwewe(ndege) huku akiongeza kuwa hakuwahi kupanda ndege, hivyo kampuni ya Betika imetimiza ndoto hiyo aliyokuwa akiiota kila siku.

Huku akisisitiza kuwa derby hiyo anategemea kupata ushindi kwa timu yake ya Yanga.

Mchezo huo utachezwa kesho saa 11 jioni katika uwanja wa Mkapa ukizikutanisha Simba iliyoko nafasi ya pili katika msimamo wa ligi kuu ikiwa na alama 60 na Yanga iliyoko kileleni ikiwa na alama 68.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles