30.4 C
Dar es Salaam
Monday, December 16, 2024

Contact us: [email protected]

Bayport yatoa milioni 15 kusaidia watoto 300 Muhimbili

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

TAASISI ya Kifedha ya Bayport Financial Services inayojihusisha na mikopo kwa watumishi wa umma, imejitolea Sh milioni 15 kusaidia gharama ya matibabu ya watoto 300 wanaotibiwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili.

Msaada huo umeenda sanjari na maadhimisho ya Siku ya Wanawake duniani yaliyoadhimishwa jana Machi 8, ambapo msaada huo umedhuhuriwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Profesa Mohamed Janabi pamoja na baadhi ya watumishi wa Bayport Financial Services Ltd.

Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Prof. Mohamed Janabi akiwa na baadhi ya watumishi wa Muhimbili na wafanyakazi wa Bayport Financial Services katika makabidhiano ya hundi yenye thamani ya Sh milioni 15 iliyotolewa na Taasisi ya Bayport kama sehemu ya msaada wa matibabu kwa watoto hospitalini hapo wenye changamoto ya gharama za matibabu. Picha na Mpigapicha wetu.

Akizungumza katika makabidhiano hayo, Mkuu wa Kitengo cha Utawala wa Bayport Financial Services, Suzan Kolimba, alisema taasisi yao imeguswa na changamoto wanazopitia watoto hali iliyowafanya wajitolee msaada huo.

Alisema tangu mwaka 2006 walipoingia kwenye sekta ya mikopo ya fedha kwa watumishi wa umma, wamekuwa wakijitolea misaada mbalimbali kama sehemu ya kurudisha fadhila kwa Watanzana waliochagua kuhudumiwa na Bayport.

“Bayport ndio taasisi ya kwanza iliyoanzisha huduma ya mikopo kwa njia ya kidijitali mwaka 2019 bila kujaza karatasi yoyote, ambapo ili mteja apate huduma yao atapiga simu ya bure 0800782700 na kupata mkopo wa haraka wa haraka.

“Hali hii inatufanya tuone thamani ya Watanzania wanaoendelea kuichagua Bayport kupata huduma za mikopo ya fedha, ndio maana tunaona haja ya kujitolea msaada wa matibabu kwa watoto hawa 300 hapa Muhimbili,” alisema Suzan.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali hiyo, Profesa Janabi, aliwashukuru Bayport kwa kitendo cha kusaidia gharama za matibabu kwa watoto hao na kuwataka waendelee kujitolea kwa jamii kwa manufaa ya Taifa.

“Huu ni msaada mkubwa kwa watoto hawa hivyo Bayport muendelee kujitolea kwenye jamii yetu kwa sababu ni jambo zuri mno mmefanya.

“Sasa wazazi na walezi wa watoto hawa angalau watakuwa wamepungukiwa na gharama za matibabu kwa sababu nyie mmejitokeza kuwasaidia,” amesema Janabi.

Huduma za mikopo ya fedha kwa watumishi wa umma kupitia Bayport zimerahishwa kutokana na mfumo wao wa kukopa kidijitaji ambapo mteja anapiga simu ya bure 0800782700 au kuingia mtandaoni www.kopabayport.co.tz kupata huduma hiyo bila kujaza makaratasi yoyote.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles