30.4 C
Dar es Salaam
Monday, December 16, 2024

Contact us: [email protected]

Naibu Waziri: Wanaofuga samaki kwenye vyanzo vya maji wafuate sheria

*Aridhishwa na uwekezaji unaofanywa na kampuni ya Tangreen Agriculture Limited inayojishughulisha kufuga samaki

Na Clara Matimo, Mwanza

Ili kulinda vyanzo vya maji na kuepusha uchafuzi wa mazingira, Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Khamis Hamza Khamis amewaagiza watu wote wanaofanya shughuli za ufugaji wa samaki karibu na vyanzo vya maji waheshimu sheria ya usimamizi wa vyanzo hivyo huku akiwaonya watakaokiuka kuchukuliwa hatua.

Sehamu ya eneo la mradi wa kufugia samaki katika Kampuni ya Tangreen Agriculture Limited iliyopo Wilaya ya Magu mkoani Mwanza.

Alitoa agizo hilo Februari 23, 2023 alipotembelea Kampuni ya Tangreen Agriculture Limited inayojishughulisha na ufugaji wa samaki aina ya sato kwa njia ya vizimba iliyopo Kijiji cha Kigangama Kata ya Kitongosima Wilaya ya Magu Mkoani Mwanza akiwa kwenye ziara ya kikazi.

Amesema uharibifu wa mazingira husababishwa kwa kiasi kikubwa na shughuli za kibinadamu ikiwemo uvuvi na ufugaji wa samaki ambazo zinafanyika ndani ya maji na zinapofanyika vyanzo hivyo vinapata changamoto.

 “Kumekuwa na utamaduni kwa baadhi ya watanzania wanaofanya shughuli hizo kwenye vyanzo vya maji au ndani ya maji wanaharibu makazi ya samaki aidha kwa kutumia uvuvi haramu, viongozi wote tusimamie sheria na utaratibu wa utunzaji wa vyanzo vya maji.  

“Watanzania wote tufanye uvuvi halali na usioharibu mazingira ambao utakuwa salama kwetu, mazingira yetu na viumbe wanaoishi ndani ya maji, sheria, sera ya mazingira na ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) ya mwaka 2020/2025  vyote vimeeleza namna ambavyo wananchi wanapaswa kuvilinda vyanzo hivyo kwa usimamizi wa serikali,”amesema Naibu Waziri Khamis na kuongeza

“Uwekezaji mlioufanya kwenye kampuni hii ni wa kisasa kabisa nimevutiwa nao endeleeni kuwekeza kadri mnavyoweza serikali iko na nyie mkiwa na changamoto tujulisheni tutazitatua maana uwekezaji huu pia unasaidia kudhibiti uvuvi haramu pia mmetoa ajira kwa vijana wetu hongereni sana,” amesema.

Mwakilishi wa Kampuni ya Tangreen Agriculture Limited inayomilikiwa na raia China Nuru Ndege amesema walianza mradi wa ufugaji  samaki mwaka 2019 uwekezaji uliofanywa unagharama zaidi ya Sh bilioni 10 lakini wamekuwa wakikabiliwa na changamoto kadhaa ikiwemo  wavuvi kuingia katika eneo la mradi kuiba na kuharibu miundombinu ya mradi, walinzi wa Kampuni kukamatwa na kushitakiwa pale wanapopambana na waharifu mbalimbali katika eneo tengefu la uwekezaji.

Ndege aliiomba Serikali iendelee kutoa elimu kwa jamii ya uvuvi juu ya uwekezaji wa vizimba ili waache kufanya shughuli za uvuvi katika eneo tengefu la mradi na kubainisha kwamba hadi sasa wana vizimba 24 vyenye vifaranga 5,000,000 na mabwawa 60 kati ya hayo 40 yanavifaranga 3,000,000.

Alisema hadi Desemba 2022 walikuwa wameishavuna tani 50 za samaki lengo ni kufikia tani 10,000 ifikapo mwaka 2024 maana wanatarajia kupanua na kuongeza eneo la uwekezaji kwa kuwa na mabwawa 120 ya kufugia vifaranga na vizimba 120 vya kufugia samaki wamedhamiria kuongeza uzalishaji mwaka hadi mwaka.

 Amesema mradi huo umekuwa na faida nyingi ikiwa ni pamonaja na kuongeza uzalishaji wa samaki aina ya sato hivyo kupunguza utegemezi wa samaki kutoka ziwani, kuendelea kutoa elimu ya ufugaji wa kisasa ili kupunguza uvuvi haramu, kukuza na kutangaza elimu ya ufugaji wa samaki ndani na nje ya nchi na kufungua fursa za ajira kwa vijana.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles