32.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 16, 2024

Contact us: [email protected]

TAWA yatekeleza maagizo ya Rais Dk. Samia ya kudhibiti wanyamapori

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania ( TAWA) imetekeleza kwa vitendo maagizo yaliyotolewa Disemba 1, 2022 na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan katika Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya UKIMWI Duniani yaliyofanyika mkoani Lindi.

Maagizo hayo ni kuhakikisha kuwa madhara yaletwayo na wanyama wakali na waharibifu yanadhibitiwa ipasavyo.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa zoezi hilo Disemba 3, 2022, Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Juma Mkomi amesema, zoezi hili la kuwavalisha tembo visukuma mawimbi litasaidia kuondoa madhara yaletwayo na wanyama hao kwa sababu, vifaa hivyo vinafuatilia mienendo ya tembo na vitawaongoza askari katika zoezi la kuwarudisha hifadhini kabla hawajafika katika makazi ya wananchi.

“Hivyo niwasihi wananchi kuendelea kuwa watulivu kwa kipindi hiki ambacho zoezi hili la uvishaji wa kola na kuwaswaga makundi ya tembo kurudi hifadhini linaendelea,” amesema Mkomi.

Naye, Kaimu Naibu Kamishna wa Uhifadhi Mlage Kabange akizungumza kwa niaba ya Kamishna wa Uhifadhi TAWA, amesema sambamba na zoezi hilo TAWA imetoa mafunzo ya kijeshi kwa vijana wanaoishi pembezoni mwa hifadhi yani Village Game Scouts (VGS) watakaotumika kama Askari wa Akiba katika kukabiliana na changamoto ya wanyama hawa hususan katika vijiji ambavyo matukio ya kuvamiwa na tembo yamekuwa yakijirudia.

Kadhalika, TAWA imenunua pikipiki ambazo zimefungwa vifaa maalumu vya kutoa matangazo kwa wananchi. Pikipiki hizo zitatumika katika maeneo ambayo magari ya doria hayawezi kuyafikia.

DCIM\100GOPRO\GOPR2443.JPG

“TAWA imekamilisha ujenzi wa nyumba za askari ambazo zimejengwa katika vijiji vya Nditi na Ngumbu vilivyopo katika wilaya za Nachingwea na Liwale. Vijiji hivi vimekuwa vikipata changamoto kubwa ya wanyama wakali na waharibifu,” amesema Kabange.

TAWA inashirikiana na Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzaniahi (TAWIRI) kwenye zoezi hilo la ufungaji wa visukuma mawimbi na la kurudisha makundi ya tembo kutoka vijiji vilivyopo Mkoani Lindi na kuwarudisha hifadhini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles