25.9 C
Dar es Salaam
Monday, December 16, 2024

Contact us: [email protected]

Migogoro yapungua sekta ya madini nchini

Na Ramadhan Hassan, Dodoma

Tume ya Madini imesema idadi ya migogoro na malalamiko katika sekta hiyo imepungua kwa kiasi kikubwa ambapo hadi kufikia Septemba, mwaka huu hakukuwa na mgogoro.

Hayo yamelezwa Oktoba 7, 2022 jijini Dodoma na Katibu Mtendaji wa tume hiyo, Yahya Samamba wakati akielezea utekelezaji wa majukumu na mafanikio ya tume hiyo.

Mtendaji huyo amesema idadi ya migogoro na malalamiko katika sekta hiyo imepungua kwa kiasi kikubwa ambapo hadi kufikia Septemba, mwaka huu hakukuwa na mgogoro.

“Katika kaguzi mbalimbali zinazofanywa na tume imeiwezesha Mamlaka ya Mapato nchini(TRA) kukusanya kodi mbalimbali kutoka migodi mikubwa na baadhi ya migodi ya kati,”amesema.

Ameitaja migodi hiyo ni wa dhahabu wa Geita, Bulyanhulyu, North Mara, Shanta Mining, Pangea Minerals Ltd, Mgodi wa almasi wa Wiliamson na Mgodi wa NIkel wa Kabanga.

Aidha, amesema ajira kwa wazawa zimefikia asilimia 97 ukilinganisha na mwaka 2018 Watanzania walikuwa ni asilimia 70.

Samamba amesema mchango wa wachimbaji wadogo kwenye mapato yanayokusanywa na tume hiyo umeimarika hadi kufikia asilimia 30 mwaka 2021 ukilinganishwa na chini ya chini ya asilimia 24 mwaka 2018.

Katibu Mtendaji huyo, amesema chini ya usimamizi wa tume, maduhuli ya Serikali yameongezeka kutoka Sh bilioni 346.275 katika mwaka 2018/19 hadi kufikia Sh bilioni 624.61 mwaka 2021/22 sawa na ongezeko la asilimia 44.5.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles