25.5 C
Dar es Salaam
Saturday, November 23, 2024

Contact us: [email protected]

Ajali mbaya yaua 10 Mbeya

Askari wa usalama barabarani na raia wakiangalia gari aina ya Toyota Hiace iliyopata ajali eneo la Mbalizi mkoani Mbeya na kusababisha vifo vya watu 10 na wengine kujeruhiwa. Picha na Pendo Fundisha
Askari wa usalama barabarani na raia wakiangalia gari aina ya Toyota Hiace iliyopata ajali eneo la Mbalizi mkoani Mbeya na kusababisha vifo vya watu 10 na wengine kujeruhiwa. Picha na Pendo Fundisha

Na Pendo Fundisha, Mbeya

WATU 10 wakiwemo watoto wadogo wawili, wamekufa papo hapo baada ya gari dogo la abiria aina ya Toyota Hiace  kulivaa lori aina ya Fuso katika eneo la Mbalizi mkoani Mbeya.

Katika ajali hiyo iliyotokea jana saa 4 asubuhi, watu saba walijeruhiwa miongoni mwao wakiwa katika hali mbaya.

Watu walioshuhudia ajali hiyo waliliambia MTANZANIA Jumamosi kuwa gari la abiria aina ya Hiace yenye namba za usajili T237 iliyokuwa ikitokea jijini Mbeya kwenda Mbalizi, ililivaa lori  aina ya T 158 CSV lililokuwa likitokea kwenye kituo cha mafuta kilichopo eneo la Mbalizi.

Wakati Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Ahmed Msangi akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo huku akisema kuwa jeshi lake linachunguza chanzo, taarifa za awali kutoka kwa mashuhuda zinaeleza ajali hiyo ilisababishwa na dereva wa Hiace ambaye alishindwa kulidhibiti gari lake lililokuwa likishuka kwenye mteremko mkali wa Mlima Mbalizi.

Maelezo ya watu mbalimbali walioshuhudia tukio hilo pia  yalionekana kumuelekezea lawama dereva wa lori ambaye walidai kuwa aliingia barabarani bila kuchukua tahadhari.

Kamanda Msangi kwa upande wake aliwataja miongoni mwa waliokufa katika ajali hiyo kuwa ni dereva wa Hiace aliyetambulika kwa jina la Petro Mngo’ngo.

Aliwataja wengine waliopoteza maisha katika ajali hiyo kuwa ni watoto wawili wa kiume, wanawake wanne na wanaume wanne.

Kwa upande wa majeruhi, Kamanda Msangi alisema wanne kati ya saba wanapatiwa matibabu katika Hospitali Teule ya Ifisi na watatu wamekimbizwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mbeya.

Gazeti hili lilifika katika Hospitali Teule ya Ifisi, ambako Muuguzi Mkuu, Sikitu Mbilinyi alilithibitishia kupokea miili 10 na majeruhi saba.

Alisema majeruhi waliopokelewa ni wanawake watatu na wanaume wanne, kati yao wanaume wawili na mwanamke mmoja walikimbizwa katika Hospitali ya Rufaa kutokana na hali zao kutokuwa nzuri.

Muuguzi huyo alisema miili ya marehemu hao imehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali hiyo ya Ifisi na kuwataka ndugu na jamaa kufika kwenye hospitali hiyo kwa ajili ya kutambua marehemu hao.

Aidha, MTANZANIA lilifanikiwa kuzungumza na kondakta wa Hiace ambaye kutokana na hali yake kutokuwa nzuri aliweza kujitambulisha jina lake kuwa ni Justin Chaula na mwingine ni Neima ambao wote wamelazwa katika hospitali hiyo ya Ifisi.

Akielezea kutokea kwa ajali hiyo, shuhuda Saidi Nzowa (44) ambaye ni dereva wa lori la mafuta Kampuni ya ASAS, alisema:

“Inavyoonyesha gari ya abiria ilifeli breki ndio maana dereva alishindwa kuisimamisha na kulivaa lori hilo ambalo lilikuwa tayari limeingia barabarani.

- Advertisement -

Related Articles

3 COMMENTS

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles