24.2 C
Dar es Salaam
Friday, November 15, 2024

Contact us: [email protected]

Wananchi Njombe waelimishwa kuhusu umuhimu wa anuani za makazi

Na Elizabeth Kilindi, Njombe

Mkuu wa Wilaya ya Njombe mkoani Njombe, Kissa Kasongwa amewaeleza wananchi wa kata ya Mtwango Halmashauri ya wilaya ya Njombe umuhimu wa zoezi la anuani za makazi kwamba utairahisishia Serikali katika mipango ya maendeleo na kutoa huduma za kijamii.

Kasongwa ameyasema hayo leo Februari 25, 2022 wakati wa uzinduzi wa zoezi hilo ndani ya halmashauri hiyo ambapo amesema serikali imejipa muda wa kuhitimisha utekelezaji wa zoezi hilo ambalo litaleta matokeo chanya kihuduma na biashara.

“Huduma zitaboreshwa hata kwenye maisha ya kawaida ambapo itakua ni rahisi kumuelekeza mtu kama una biashara au una mzigo pamoja na kupunguza matukio ya kihalifu,”amesema Kasongwa.

Kasongwa amesema zoezi hilo limekuja wakati sahihi nchi ikiwa inajiandaa na zoezi la sensa ya watu na makazi itakayofanyika baadaye mwaka huu.

“Zoezi hili limekuja wakati sahihi kabisa kwa sababu tuna zoezi la sensa kwa hiyo vyote vinakwenda sambamba. Nimpongeze sana Rais Samia Suluhu Hassan tunaahidi kwamba tutafanya zoezi hili kwa umakini, ufanisi na tutakamilisha kwa wakati kulingana na maelekezo ya serikali kuu,” amesema Kasongwa.

Pia katika hatua nyingine amewataka wananchi kuchukua taadhari ya ugonjwa wa Uviko-19 kwa sababu bado upo.

“Ugonjwa wa Uviko-19 bado upo, hivyo niwasihi sana ndugu zangu ambao hawajapata chanjo wakachanje ili kuwa salama,”amesema Kasongwa.

Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Njombe Sharifa Nabalang’anya amesema zoezi la anuani za makazi ni utekekezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles