KOCHA wa klabu ya Liverpool, Jurgen Klopp, amesisitiza kuhamishia nguvu zake katika michuano ya Europa League ili kujihakikishia nafasi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.
Klabu hiyo kwa sasa inashika nafasi ya nane katika msimamo wa Ligi, huku ikiwa na alama 38 baada ya kucheza michezo 26, lakini kocha huyo amesema lengo lake ni kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao, hivyo lazima ajitume katika michuano ya Europa.
“Kuna baadhi ya klabu kwa sasa mawazo yao ni kushinda Europa, nadhani sisi ni miongoni mwa timu hizo ambazo zinahitaji kushinda Ligi hiyo.
“Sina la kusema zaidi, ila ukweli ni kwamba tuna lengo hilo la kushinda kwa ajili ya kujihakikishia tunashiriki Ligi ya Mabingwa, japokuwa si kazi ndogo kufanikiwa kwa hilo,” alisema Klopp.
Hata hivyo, Klopp amesema kwamba bado ana nafasi ya kupanda nafasi za juu katika Ligi Kuu nchini England msimu huu na akiwa na matumaini makubwa ya kuleta ushindani msimu ujao.