NYOTA wa zamani wa klabu ya Chelsea na timu ya Taifa ya Ivory Coast, Didier Drogba, ameonekana kumtetea mchezaji mwenzake raia wa Ivory Coast ambaye anakipiga katika klabu ya PSG, Serge Aurier, kwa kitendo cha utovu wa nidhamu kwa kocha wake.
Beki huyo wa PSG aliweka video kwenye mitandao ya kijamii ambayo ilimuonesha akidai kwamba kocha wake, Laurent Blanc na mshambuliaji Zlatan Ibrahimovic wana dharau.
Kutokana na video huyo, kocha aliamua kuchukua maamuzi ya kumuweka benchi mchezaji huyo katika mchezo dhidi ya Chelsea mwanzoni mwa wiki hii katika Ligi ya Mabingwa ambapo PSG ilishinda mabao 2-1.
Kusimamishwa kwa mchezaji huyo kumemgusa sana mshambuliaji wa timu ya Montreal Impact, Drogba, na kudai kwamba maamuzi ya kocha huyo yamekuwa makubwa na hayana ufundisho kwa mchezaji.