26.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 23, 2024

Contact us: [email protected]

Mradi wa umwagiliaji kuhudumia wananchi 2000 Mwanga

Safina Sarwatt, Mwanga

SERIKALI imetoa zaidi ya bilion moja ya mradi wa sikimu ya kilimo cha umwagiliaji ya kambi ya swala katika kijiji cha Kirya wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro utakao nufaisha wananchi 2000.

Akizungumza katika ziara ya kukagua miundombinu ya mradi huo ikiwa ni pamoja na mkukabidhi rasmi mkandarasi kwa utekelezaji, Kaimu Mkurugenzi wa uboreshaji wa miundombinu ya umwagiliaji kutoka tume ya Taifa umwagiliaji, Mhandisi Tonda Kimasa amesema wananchi watakao nufaika ni kutoka vijiji vya Kirya Wilaya ya Mwanga pamoja baadhi ya vijiji vya wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara ambapo utatekelezwa kwa muda miezi minane.

“Mradi huu unatakelezwa kwa fedha za ndani na mradi unatekelezwa kwa muda wa miezi minane kuanzi sasa ambapo ni upanuzi mashamba kutoka hekta 450 hadi kufikia hekta 900 , usakafiaji wa mifereji wenye urefu wa kilometa tatu,Ujenzi wa barabara za mashambani kilometa tano pamoja na vigawa maji vinne,”amesema.

Mhandisi wa umwagiliaji Mkoa wa Kilimanjaro, Saidi Ibrahim amesema mkoa  huo unajumla ya mifereji ya asili ya skimu za umwagiliaji 247, miradi 32 zimeboreshwa lakini katika mpango wa uboreshaji wa miundombinu ya umwagiliaji skimu mbalimbali zinaendelea kuboreshwa.

“Katika mwaka huu wa fedha na mwaka uliopita wa fedha miradi mbalimbali ziliboreshwa na leo tumekabidhi mradi wa skimu ya umwagiliaji Kirya kambi ya swala wenye thamani ya zaidi ya bilioni moja umekabidhiwa kwa mkandarasi,”amesema.

Baadhi ya Wananchi wameishukuru serikali kutoa fedha kwa ajili ya ukamilishaji wa mradi huo na kwamba utawasaidia kuongeza mapato na kujikwamua kiuchumi huko ameishauri serikali kuweka vivuko vya mifungo.

Mwanakamati wa mradi kilimo cha skimu ya umwagiliaji kambi ya Swala, Petro Mussa, amesema katika utekelezaji wa mradi huo kuzingatiwe uwekaji wa madaraja kutokana na eneo hilo kuwa na mifugo.

Upendo Msola amesema mradi huo ni fursa kubwa kwa wanawake kwani utawasaidia kujikwamua kiuchumi na kufungua fursa nyingi za ajira na kuondokana na hali ya umaskini.

Mradi huo ni fursa kubwa kwa wanawake na kwamba wamesubiri  kwa muda mrefu kutokana na kwamba kipindi cha nyuma walikuwa wanashindwa kulima kwani maji yalikuwa hayafiki kwenye mashamba yao.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga Mwajuma Nasombe namshukuru mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuleta fedha ziadi ya billion moja na kuwataka wananchi kulinda mradi huo ili uwe endelevu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles