29.9 C
Dar es Salaam
Sunday, November 17, 2024

Contact us: [email protected]

Taasisi zaombwa kuambatanisha elimu ya uzazi na ujasiriamali

Na Yohana Paul, Geita

Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Geita, Last Lingson ametoa wito kwa Taasisi za Serikali na Mashirika ya Yasiyo ya Kiserikali (NGOs) zinazojihusisha na utoaji wa elimu ya afya ya uzazi na uzazi wa mpango kwa vijana kuambatanisha elimu hiyo na elimu ya ujasiriamali.

Lingson alisema hayo katika mahojiano maalumu na Mtanzania Digital na kueleza kuwa kwa hali na mwenendo wa maisha ya sasa, njia sahihi ya kwa vijana kuwasaidia ni kuwapatia elimu ya uzazi wa mpango na elimu ya mikopo na ujasiliamali kwani changamoto za kiuchumi zimekuwa na mchango mkubwa kupelekea mimba za utotoni.

Afisa Ustawi wa Jamii Mkoa wa Geita, Last Lingson (Katikati) akizungumuza na wananchi wilayani Bukombe Mkoani Geita.

Alisema ni ukweli ulio wazi kwamba mkoa wa Geita vijana wengi wamejitahidi kufuata elimu ya uzazi lakini suala la umasikini limekuwa kikwazo kwao na wanapopatia vishawishi vya kifedha wengi wamejikuta wanaingia kwenye vishawishi na kuishia katika tamalaki ya magonjwa ya zinaa na mimba zisizotarajiwa.

“Unapompatia kijana elimu ya afya ya uzazi na elimu ya mikopo ataweza kufanya ujasiliamali huku akitambua kuhusu mabadiliko ya kimwili na kiuzazi na atakuwa imara kwenye masuala ya kiuchumi hivyo kundi hili litakuwa imara zaidi na sisi kama jamii na taifa tutaweza kufikia mahala pazuri zaidi,” anasema.

Aidha Lingson alitoa wito kwa vijana wa kiume kutilia mkazo suala la elimu ya uzazi kwani wengi wao wamekuwa wakipuuzia kwa kuamini elimu hiyo inawahusu zaidi vijana wa kike dhana ambayo ni potofu na inapaswa kufutwa kwani vijana wa kiume nao wamekuwa chanzo za mimba za utotoni kwa kujua ama kutokujua.

Kwa upande wake Afisa Maendeleo Vijana Halmashaurii ya mji wa Geita, Zengo Pole aliomba vijana kuwekea mkazo elimu ya uzazi inayotolewa na mashiry, taasisi na wataalamu wa afya kupitia warsha na vyombo vya habari kwani itawawezesha kupiga hatua za kimaendeleo na kufikia malengo yao.

Zengo alisema ni ukweli ulio wazi kijana ili afikie malengo yake ni lazima aangalie suala la afya ya uzazi ili kuhakikisha anajilinda na kupanga na pale anapotaka kuoa au kuolewa ajaribu kujiwekea malengo yake juu ya idadi ya watoto anaoweza kuwamudu katika malezi.

“Elimu hii itawasaidia vijana kujitathimini uwezo wao, namna ya kuweza kuhimili kulea familia ingawa tunaamini watoto ndiyo nguvu kazi ndani ya familia, lakini ni lazima kuwe na mipango kwamba wanazaa watoto wangapi wanawamudu, ili kuondoa changamoto za kuzaa watoto kiholela na kuongeza idadi kubwa ya watoto wa mitaani,” anasisitiza,” alisema.

Alieleza kuwa jamii kutozingatia elimu ya afya ya uzazi imepelekea ongezeko la watoto wa mitaani kutokana na watu wengi ikiwemo vijana kuzaa bila malengo na kuwaacha watoto waende wanakokujua jambo ambalo linatoa ulazima wa kuweka mipango ya kuzaaa, kulinda, kutunza na kuhudumia watoto kabla na baada ya ndoa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles