29.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 16, 2024

Contact us: [email protected]

Paroko: Ni jukumu la jamii kuwasaidia watoto wenye ulemavu

Na Victor Mkinda, Morogoro

 Wito umetolewa kwa jamii ya Watanzania kuwasaidia  watoto wenye ulemavu na wale wanaoishi kwenye mazingira magumu.

 Wito huo umetolewa mwishoni mwa wiki na Paroko wa Parokia ya Mtakatifu Gonzaga Mvomero, jimbo Katoliki la Morogoro, Herman Kiangazi wakati wa tamasha la usiku wa mwangaza, tamasha mahususu kwa ajili ya kuwaenzi watoto wenye ulemavu.

Kiangazi amesema kuwa watoto ni Baraka kutoka kwa Mungu, hivyo sisi wanadamu tunatakiwa kuzipokea baraka hizo kutoka kwa Mungu pasipo ubaguzi ya kuwa huyu ni mlemavu ama lah.

“Binadamu wote ni sawa, hali kadharika watoto wote ni sawa, tusiwabague watoto wenye ulemavu bali kama jamii tunapaswa kuwapenda, kuwasaidia, kuwaongoza na kuhakikisha kuwa wanapata mahitaji yote muhimu ikiwa ni pamoja na elimu na ustawi wa afya zao,” amesema Kiangazi.

Kiangazi aliongeza kusema kuwa ni vema jamii ikatupia jicho juu ya madhira yanayowapata watoto wenye ulemavu na wanaoishi kwenye mazingira magumu ili waweze kuishi kama wanavyoishi watoto wengine na kusaidiwa kufikia ndoto zao.

Akizungumza kwenye tamasha hilo, Mkurugenzi wa taasisi ya kulelea watoto wenye ulemavu wa akili na viungo ya EMFERD, Josephine Bakhita, alisema kuwa jamii inapaswa kufahamu kuwa ulemavu sio kushindwa bali ni maumbile tu.

“Ulemavu sio kushindwa kila kitu. Watu wenye ulemavu wakiwezeshwa wanaweza kufanya mambo ambayo hata sisi tulio wazima hatuwezi”. alisema Bakhita.

Bakhita alisema kuwa ni vema jamii ikaondoa mtazamo hasi juu ya wenye ulemavu kuwa hawawezi chochote, kinyume chake wanapaswa kuwasadia kupata elimu na ujuzi wa aina mbali mbali ili  waweze kupata ustawi na kuepukana na utegemezi kwa kujisaidia wenyewe.

“Wapo wenye ulemavu ambao wana vipaji, ujuzi na maarifa makubwa, hao wanachagia pato la familia na jamii kwa ujumla. Ni jukumu letu sisi tusio na ulemavu, kila mmoja kwa nafasi yake, kuondokana na mtazamo hasi juu ya ulemavu na kuwasaidia watu wenye ulemavu ili waweze kujisaidia wenyewe,” alisema Bakhita.

Akielezea kuhusu tamasha la usiku wa mwangaza, Bakhita alisema kuwa tamasha hilo hufanyika kila mwaka mahususi kuihamasisha jamii kuwaenzi na kuwapa nafasi ya heshima watu wenye ulemavu  huku likiwa linafadhiriwa na mcheza kikapu maarufu wa nchini Marekani, Tim Tabew.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles