29.9 C
Dar es Salaam
Monday, December 16, 2024

Contact us: [email protected]

Stars yajazwa mamilioni ikikwea kwenda CHAN

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Abdallah Ulega akimkabidhi Nahodha wa timu ya Taifa ( Taifa Stars), John Bocco fedha za posho za ndani za wachezaji pamoja na bonasi ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Congo DRC Sh milioni 60, ikiwa ni sehemu ya mchango wa Serikali kusaidia maandalizi ya timu hiyo kuelekea mashindano ya CHAN 2021 nchini Cameroon.

Makabidhiano hayo yamefanyika usiku wa kuamkia leo katika hafla ya kuiaga timu hiyo katika Hoteli ya Tiffany jijini Dar es Salaam, Naibu Waziri Ulega pia aliwakabidhi viongozi pamoja na wachezaji wa timu bendera ya Taifa.

“Serikali imechangia zaidi ya Sh milioni 60 kama bonasi na posho za ndani za wachezaji na benchi la ufundi, bado tunapambana kupata fedha ili kusaidia katika maeneo mengine, TFF hakikisheni mnasimamia nidhamu ya matumizi ya fedha hizi pamoja na nidhamu kwa vijana ili timu yetu iweze kutuwakilisha vyema,” alisisitiza Ulega.

Taifa Stars imeondoa leo alfajiri kuelekea nchini Cameroon kushiriki michuano ya CHAN 2021.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles