25.8 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

11 WAFARIKI DUNIA KWA AJALI, JPM AWALILIA


Na RENATHA KIPAKA, BIHARAMULO

WATU 11 wamefariki dunia na wengine sita kujeruhiwa kutokana na ajali ya gari ya abiria ya hiace kugongana na malori mawili katika Kijiji cha Mubigera Kata ya Nyantakara wilayani Biharamulo Mkoa wa Kagera.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kagera, Agustini Ollomi alisema ajali hiyo ilitokea juzi saa11:12 jioni.

Alisema  gari hilo la abiria  la hiace  lililipita kwa kasi gari lililokuwa mbele yake na kugongana na gari jingine.

Kamanda Ollomi alisema baada ya kulipita kwa mbele lori la kwanza    ambalo lilikuwa linavuta trela,   dereva wa gari la abiria alishindwa kulimudu na kuligonga lori jingine ambalo pia lilikuwa linavuta trela.

Alisema kuwa  ajali  hiyo ilisababisha vifo cha watu wanane akiwamo dereva na kufanya idadi ya waliokufa    papo hapo kwenye ajali hiyo kufikia saba.

Wawili walifia njiani wakipelekwa hospitali kabla ya kuongezeka wengine wawili waliofariki dunia wakati wakipatiwa matibabu katika Hospitali Teule ya Biharamulo.

Mmoja wa abiria alimueleza Kamanda Ollomi kuwa  chanzo cha ajali ni dereva wa hiace ambaye alionywa na abiria kuacha kuzipita gari nyingine akiwa mwendo kasi lakini hakuwasikiliza.

Ollomi aliwataja majeruhi kuwa ni Juma Samu (22) mkazi wa Nyampalahala Runzewe, Joseph Otieno (32) raia wa Kenya, Oscar Sebastian(27) wa Ruhinga Kibondo, Baseka Mashinga (31) kutoka Kibondo , Mahururo Charles (25) wa Kakonko.

Kamanda   alisema   majeruhi hao wanaendelea na matibabun na afya zao zinaendelea vizuri.

Mganga Mkuu wa Hospitali Teule ya Biharamulo, Dk. Grasmus Sebuyoya alithibitisha kupokea miili  hiyo na majeruhi kadhaa.

Wakati huo huo, Rais Dk John Magufuli amemtumia salamu za rambirambi Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Meja Jenerali Mstaafu, Salum Kijuu kutokana na ajali hiyo.

Taarifa ya Ikulu iliyotolewa jana na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU  Gerson Msigwa ilisema  Rais Magufuli alipokea kwa huzuni na masikitiko makubwa taarifa za vifo vya Watanzania hao.

Alimtaka Meja Jenerali Mstaafu Kijuu kumfikishia pole kwa familia za marehemu wote, ndugu, jamaa, marafiki na wote walioguswa na vifo hivyo.

“Nimehuzunishwa na kusikitishwa na vifo hivi, nawapa pole wafiwa wote, ninawaombea marehemu wapumzike mahali pema na majeruhi wapone haraka  i waweze kuungana na familia zao na kuendelea na shughuli zao za kila siku,” alisema Rais Magufuli.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles