29.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 17, 2024

Contact us: [email protected]

Urusi nayo yajitoa mkataba wa silaha hatari

MOSCOW,Urusi

SERIKALI ya hapa  imejiondoa katika mkataba wa kupinga uundaji wa makombora ya masafa marefu uliyofikiwa enzi ya vita baridi kufutia uamuzi uliochukuliwa na Marekani.

Marekani ambayo kwa muda mrefu imekuwa ikiilaumu Urusi kwa kukiuka mkataba huo ilitangaza kusitisha rasmi wajibu wake mwishoni mwa wiki.

Akizungumza juzi mjini hapa, kiongozi wa nchi hii, Rais Vladimir Putin alisema taifa hili litaanza kuunda makombora mapya na akaonya endapo  Marekani itatengeneza makombora na wao watafanya hivyo.

Mkataba huo uliofikiwa kati ya Marekani na muungano   wa Jamhuri ya Kisovieti na kutiwa saini mwaka 1987 ulipiga marufuku mataifa yote dhidi ya matumizi ya makombora ya masafa mafupi na yale ya kadri.

“Washirika wetu wa Marekani wametangaza kusitisha wajibu wao katika mkataba huo nasi pia tunafuata mkondo wao,”alisema Rais Putin.

Katibu mkuu wa muungano wa kijeshi wa mataifa ya Magharibi Nato, Jens Stoltenberg alisema kwamba washirika wote Ulaya yanaunga mkono hatua ya Marekani kwa sababu Urusi imekiuka mkataba huo kwa miaka kadhaa.

Alisema matakwa ya miezi sita iliyotolewa na Marekani kwa Urusi kufuata kutekeleza kikamilifu yanafaa kuzingatiwa.

Rais wa Putin aidha alisema tuhuma za Nato dhidi ya taifa lake ni kisingizio cha Marekani kujiondoa katika mkataba huo.

Marekani inasema ina ushahidi kuwa makombora mapya yaliyoundwa na nchi hii  ni moja ya  yaliyopigwa marufuku katika mkataba wa INF.

Baadhi ya maofisa wa Marekani wanasema kuwa makombora ya aina ya 9M729 – yanayotambuliwa na Nato kama SSC-8 tayari yameanza kutumika.

Mwezi Disemba mwaka jana, Rais wa Marekani Donald Trump, aligusia kuwa taifa hilo huenda likajiondoa katika mkataba wa INF ikiwa Urusi haitabadili msimamo wake.

Katika mkutano huo wa juzi akiwa ameandamana na  mawaziri wake ulinzi na wa mambo ya nje, Rais Putin alisema wataanza kuunda silaha mpya ikiwa ni pamoja na makombora ya kulipua meli na mengine yaliyo na kasi ya mara tano zaidi ya mlio wa sauti.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles