24.2 C
Dar es Salaam
Friday, November 15, 2024

Contact us: [email protected]

Netanyahu azuru Brazil

RIO DE JANEIRO, BRAZIL

RAIS mteule wa Brazil mwenye siasa kali za mrengo wa kulia Jair Bolsonaro jana alikutana kwa mara ya kwanza na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu mjini Rio de Janeiro na kukubaliana kuongeza ushirikiano baina ya nchi zao.

Licha ya kukutana na kufanya mazungumzo  baina ya viongozi hao wawili, lakini hakuna tangazo lililotolewa kama ilivyotarajiwa na baadhi ya watu kuhusu kuhamisha ubalozi wa Brazil na kupeleka mjini Jerusalem.

Ziara hiyo inamfanya Benjamin Netanyahu kuwa waziri mkuu wa kwanza wa Israel kuitembelea Brazil na kukutana na rais Bolsonaro ambaye atachukua rasmi madaraka kuanzia Januari mosi baada ya kushinda uchaguzi wa Oktoba.

Bolsonaro na maafisa wake wakuu wamesema mara kadhaa kwamba watahamisha ubalozi wa Brazil kutoka mjini Tel Aviv na kupeleka Jerusalem. Lakini tangu kuchaguliwa kwake ameshinikizwa hasa na wadau katika sekta ya kilimo wanaohisi kwamba uamuzi huo utayarudisha chini mauzo yao ya nyama ambayo ni halali katika mataifa ya Kiarabu.

Kulingana na barua iliyoonekana na shirika la habari la Reuters mapema Desemba, muungano wa nchi za kiarabu ulimwambia rais huyo mteule kwamba kuuhamisha ubalozi huo kutaathiri uhusiano wa nchi yake nya nchi za Kiarabu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles