30.4 C
Dar es Salaam
Monday, December 16, 2024

Contact us: [email protected]

Aunt awashangaa mashabiki zake

JENNIFER ULLEMBO-DAR ES SALAAM

MWIGIZAJI wa filamu Tanzania, Aunt Ezekiel, ameshangaa mashabiki ambao wamekuwa wakitumia muda mwingi kujadili mwili wake.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Aunt alisema ameamua kujipunguza ili kujiepusha na maradhi mbalimbali yanayosababishwa na uzito mkubwa.

Alisema kila mtu anauwezo wa kutimiza malengo aliyojiwekea, hivyo hata upande wake suala la kupungua lilikuwa la muda mrefu sana.

“Mashabiki wamekuwa wakinijadili sana, ukweli sifurahishwi nikiwa kama kioo cha jamii sioni kosa kuamua kupunguza uzito, kwani hiyo ni njia ya kunisaidia kujikinga na magonjwa tofauti,” alisema Aunt.

Aunt alisema mashabiki wanatakiwa kumkosoa pale anapofanya makosa katika kazi zake au matukio ambayo hayana mafundisho kwa jamii.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles