29.2 C
Dar es Salaam
Friday, November 15, 2024

Contact us: [email protected]

MAN CITY WAWEKA HISTORIA NYUMBANI

MANCHESTER, ENGLAND


KLABU ya Manchester City, imeweka rekodi ya kushinda michezo 16 mfululizo kwenye uwanja wa nyumbani na kuifikia rekodi ambayo waliiweka miaka 100 iliyopita.

Kikosi hicho cha kocha Pep Guardiola, kimeweka historia hiyo juzi baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya wapinzani wao Bristol City, kwenye michuano ya Kombe la Carabao hatua ya nusu fainali.

Klabu hiyo ya Manchester City iliwahi kufanya hivyo kwenye msimu wa mwaka 1920-21, hivyo chini ya kocha wao, Guardiola imeweza kufanya hivyo msimu huu.

Katika mchezo huo wa juzi, Man City walikuwa na kibarua kigumu dhidi ya wapinzani hao ambao wanaonekana kuleta upinzani mkubwa kwenye michuano hiyo msimu huu. Bristol City walikuwa wa kwanza kupata bao katika dakika 44 kupitia kwa mchezaji wao Bobby Reid kwa mkwaju wa penalti.

Hadi dakika 45 zinamalizika, klabu hiyo ilikuwa mbele kwa bao 1-0, lakini baada ya kupindi cha pili kuanza, Man City waliingia kwa mipango hivyo waliweza kupata bao la kusawazisha katika dakika ya 55 kupitia kiungo wao mshambuliaji, Kevin De Bruyne.

Ushindani uliendelea kuwa wa hali ya juu huku kila timu ikionekana kutafuta bao la kuongoza, hivyo katika dakika za majeruhi Man City waliweza kuzizima kelele za wapinzani wao kupitia mshambuliaji wao, Sergio Aguero na kuifanya timu hiyo iweke historia kwenye uwanja wa nyumbani.

Manchester City ambao ni vinara wa Ligi Kuu nchini England, wiki hii wanatarajia kufunga safari hadi kwenye Uwanja wa Anfield kupambana na wapinzani wao Liverpool ambao wanashika nafasi ya nne kwenye msimamo. Manchester wanashika nafasi ya kwanza wakiwa na pointi 62 wakifuatiwa na wapinzani wao Man United wakiwa na pointi 47 baada ya kucheza michezo 22.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles