26.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Array

Zungu: Wataalamu fanyeni tathmini ya mazingira

MWANDISHI WETU – DAR ES SALAAM

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira),  Mussa Azzan Zungu amewataka wataalamu wa mazingira kufanya tathmini ya mazingira katika maeneo ya bahari kupata dawa ya madhara yanayotokana na mabadiliko ya tabianchi.

Zungu alitoa kauli hiyo alipofanya ziara katika eneo la bahari lenye mgogoro kati ya Motison wanaomiliki hoteli ya Whitesand wakituhumiwa na wamiliki wa hoteli ya Wellworth Kunduchi kwa kujenga ukuta baharini hatua iliyosababisha maji kujaa hotelini kwao.

Akizungumza katika eneo hilo akiwa ameambatana na watendaji kutoka Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) waziri huyo aliwataka kuwa wavumilivu kusubiriwa wataalamu wa sayansi ya bahari wafanyie kazi na kutoa majibu wiki hii.

Hata hivyo Waziri Zungu aliwataka wananchi kuacha tabia ya kukata miti ovyo kwani ndio sababu kubwa ya maji ya bahari kujaa isivyo kawaida na kuingia katika maeneo yao.

“Leo tunatazama mgogoro wa watu wawili kesho tutakuwa na wa watu watano au sita, tupeni muda nimekuja hapa na mkurugenzi wa NEMC na wataalamu wake kutazama na dawa ya changamoto tunayo kwa hiyo wiki ijayo tutawaita na tutawaambia tulichofanya kuhakikusha kila mtu ana amani ndiyo kazi ya Serikali,” alisema.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa NEMC, Dk. Samuel Gwamaka aliwataka wawekezaji wote kufanya tathmni ya athari za mazingira (EIA) ili kuepusha migogoro isiyokuwa ya lazima,

Alisema kuwa binadamu tunaishi kwa kutegemeana kwenye mazingira na ndiyo maana NEMC haitoi cheti hadi ifanyike tathmnini hiyo kubaini madshara yanayoweza kutokea kwa wananchi kupitia uwekezaji unaofanyika.

“Natoa rai kwa wawekezaji wote wawe wa viwanda ama htoeli katika fukwe zetu kufanya tathmni na kupitia tathmini hiyo tutapata maoni kutoka kwa watu wanaokuzunguka kujua je uwekezaji wako unawaathiri vipi na kama kuna athari ndogo tunajua namna ya kuzitatua ili kuepusha migioogoro,” alisisitiza.

Akitoa maoni yake kuhusu changamoto hizo Mtaalamu wa Sayansi ya Bahari, Rose Mtui alisema kuwa suluhisho ni kuotesha mikoko ambayo inalunda fukwe zikibomoke kutokana na mmomonyoko wa udongo.

Aliongeza kuwa uchimbaji mchanga holela katika kingo za miti na uvuvi haramu unachangaia changamoto za kimazingira katika fukwe za bahari kwani unaharibu matumbawe ambayo yakiharibika mawimbi ya bahari higonga moja kwa moja na kwa kasi fukwe na hivyo maji kujaa kupita kiasi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles