27.1 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Zungu: Ninawapuuza wasaka tonge Ilala

ZunguNa Adam Mkwepu, Dar es Salaam

MBUNGE wa Ilala, Mussa Azzan Zungu (CCM), amesema hana muda wa kulumbana na wanasiasa wanaotafuta ubunge kwa kutumia jina lake hasa kwa Ilala.

Amesema hatarudi nyuma kuwatumikia wapiga kura wake na sasa amejikita kuhakikisha anasimamia kutekelezaji Ilani ya Uchaguzi wa CCM na si kubishana na watu wanaotafuta ubunge kwa kutumia mitandao ya jamii ikiwamo facebook.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Zungu alisema kwa siku kadhaa watu watu wasioitakia mema Ilala wamekuwa wakitumia mitandao ya jamii kuchapisha vijarida kwa lengo la kumchafua mbele ya wapiga kura wake jambo ambalo amesema hawawezi kufanikiwa.

“Unajua kuna mambo yanastaabisha sana… kuna watu ambao ni wasaka tonge wanahaha usiku na mchana eti wamchafue Zungu; mara amekula fedha za Mfuko wa Jimbo Sh milioni 400. Tena hiki kijarida kilitoa taarifa hii mwaka 2012 na sasa wanahangaika wanaitoa tena sasa mwaka 2015. Ninachotaka kusema jimbo letu hatuwezi kupata kiasi hicho cha fedha kwa sababu idadi ya watu si kubwa.

“Hizi fedha huwa zinatolewa kwa kigezo na hata matumizi yake huwa yanapangwa na kamati maalumu ambayo mbunge ni mwenyekiti tu na huwezi kuzikuta katika akaunti ya mbunge ila zinaingia katika halmashauri.

“…matumizi ni pamoja na kupanga matumizi ya miradi ya maendeleo lakini mwisho wa siku Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) huzikagua. Je, ni wapi Zungu anahusika, huu ni wakati wa uchaguzi Watanzania watarajie kuyaona mengi kutoka kwa wasaka tonge,” alisema Zungu.

Alisema pamoja na hatua hiyo lakini hatayumba kutekeleza ilani ya uchaguzi kwa wapiga kura wake.
Zungu aliwataka wanasiasa wanaomezea mate jimbo la Ilala wasiwe na hofu muda ukifika wakutane uwanjani kwa sababu waamuzi wa mwisho ni wapiga kura.

“Wananchi ndiyo waamuzi wa mwisho… eti unakutana na mwanasiasa uchwara tena msaka tonge anahaha kutaka kutafuta umaarufu kwa kutumia jina la Zungu, hofu ya nini kama unajiamini subiri wakati,” alisema Mbunge huyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles