25.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

ZUMA: NILIZOMEWA SABABU YA UWAPO WA DEMOKRASIA AFRIKA KUSINI

PRETORIA, AFRIKA KUSINI


RAIS wa Afrika Kusini Jacob Zuma amesema hana tatizo baada ya kuzomewa wakati wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wafanyakazi akisema nchi hii ni ya demokrasia, si kiimla.

“Utakubaliana nami kuwa katika nchi yenye viongozi wa kiimla, hakutakuwa na maandamano wala kuzomea,” Zuma aliwaambia waandishi wa habari.

Katika nchi isiyo na demokrasia, kutakuwa na rais mwenye hasira akiamrisha polisi kuwakamata watu hawa, alisema.

Wakati wa siku hiyo, Wafanyakazi walimkemea  Zuma na kumtaka ajiuzulu.

Akijibu hilo, Zuma alisema, "Nina furaha kuwa watu wa Afrika Kusini wamekomaa kidemokrasia na wana rais ambaye wanaweza kumzungumzia chochote walicho nacho akilini mwao.”

Alionekana kupuuzia mbali uwezekano wa kuondoka madarakani, akisema kuwa katika nchi yenye demokrasia viongozi hupigiwa kura kuingia na kuondoka madarakani.

Zuma amekuwa chini ya shinikizo kutoka kwa makundi mbalimbali  vikiwemo vyama vya wafanyakazi, biashara kubwa, vyama vya upinzani na wanachama wa chama chake kumtaka ajiuzulu.

Amekuwa akiandamwa na mlolongo wa kashfa za ufisadi wakati wa kipindi chake madarakani na kushutumiwa baada ya kumfuta waziri wake wa fedha aliyekuwa akiheshimiwa nchini humo Machi mwaka huu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles