23.7 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Zuma hatihati kutimuliwa ANC

Jacob Zuma
Jacob Zuma

JOHANNESBURG, AFRIKA KUSINI

CHAMA tawala nchini hapa, African National Congress (ANC), kinafikiria kufanya mkutano wa mapema kubadili uongozi wake wa juu baada ya kufanya vibaya zaidi katika uchaguzi, ikiwa mara ya kwanza tangu kumalizika kwa utawala wa ubaguzi wa rangi miaka 22 iliyopita.

Mkutano wa kuchagua mrithi wa kiongozi wa chama hicho, Rais Jacob Zuma, ulipangwa kufanyika Desemba 2017, lakini maofisa wa ANC wamesema mazungumzo yako njiani ili ufanyike mapema zaidi.

Lengo la kufanya hivyo ni kupata muda zaidi wa kujipanga upya baada ya matokeo mabaya waliyopata katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na kujiandaa kwa uchaguzi wa kitaifa mwaka 2019.

Hata hivyo, chama hicho kilipata ushindi wa jumla wakati wa uchaguzi huo uliofanyika Agosti 3, mwaka huu.

Lakini sifa mbaya zinazokiandama, za tuhuma za rushwa dhidi ya Zuma, kiwango kikubwa cha ukosefu wa ajira na mporomoko wa uchumi, zilisababisha kupoteza uungwaji mkono mkubwa, hasa katika majiji makubwa.

Hata hivyo, wachambuzi wa mambo wanasema haijulikani wazi iwapo mkutano huo utamwondoa Zuma au maofisa wengine waandamizi, ambao ni wakosoaji wakubwa wa rais huyo.

Umoja wa Vijana wa ANC (ANCYL), ambao ndio ulioasisi wazo hilo la mkutano wa mapema, ni ngome ya Zuma ndani ya chama.

Zuma mwenyewe ameweka wazi kuwa hatawania urais kwa muhula wa tatu, lakini katiba ya chama haimzuii kufanya hivyo.

“Wazo la uchaguzi wa mapema si baya, kwa sababu litaupa uongozi muda wa kutosha kujiandaa kwa uchaguzi mkuu wa mwaka 2019,” Katibu Mkuu wa ANC, Gwede Mantashe, aliuambia mkutano wa wanahabari ingawa hakutoa uhakikisho wa lini uamuzi huo utafanywa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles