KAMPUNI ya ving’amuzi ya Zuku imesema itaendelea kuboresha sekta ya filamu nchini kwa kutangaza kazi za wasanii ndani na nje ya nchi.
Mkuu wa kampuni hiyo nchini, Omari Zuberi, alisema hayo jana wakati wa uzinduzi wa kifurushi kipya cha Smart.
“Kazi yetu ni kuwatangaza wasanii nje na ndani ya nchi kupitia Zuku filamu kwa kuwa tunaamini kwamba kundi hili linapaswa kuinuliwa ili waweze kupata masilahi ya kutosha kutokana na kazi zao,” alisema Zuberi.
Kampuni hiyo ambayo ni mdhamini wa tamasha kubwa la filamu za kimataifa litakalofanyika visiwani Zanzibar, kwa sasa kifurushi hicho kipya kitakuwa kikilipiwa Sh 10,000 zitakuwa na chanel zaidi ya 20.