22.7 C
Dar es Salaam
Sunday, June 4, 2023

Contact us: [email protected]

Zuchu kuwakutanisha wasanii wa Bara na Zanzibar

Na Brighiter Masaki, Darv es Salaam

Msanii wa Bongo Fleva nchini, Zuhura Othuman, ‘Zuchu’ anatarajia kufanya tamasha la ‘Zuchu Home Coming’ Agosti 21, mwaka huu katika uwanja wa Amani, Unguja visiwani Zanzibar.

Akizungumza na Mtanzania Digital, Zuchu amesema kuwa tangu ametambulishwa rasmi na lebo ya ya Wasafi amekuwa na shauku kubwa ya kutaka kufanya tamasha litakalowashirikisha wasanii wa visiwa hivyo na wengine kutoka Bara.

Zuchu amesema sababu iliyomfanya kwenda kufanya tamasha hilo Zanzibar ilitokana na tamasha lake la kwanza alilolifanya katika ukumbi wa Mlimani City ‘I am Zuchu’ kuwa kubwa na lililovutia watu wengi na kuonyesha nia na dhumuni la sanaa anayoifanya.

“Wote tunafahamu kwenye utafutaji unaweza kuishi popote lakini hii hainibagui kwamba mimi ni Mtanzania lakini nimetokea Zanzibar na nimekulia hapa,” amesema Zuchu.

Mkali huyo wa wimbo Sukari, ametaja sababu za kuita tamasha lake ‘Zuchu Home Coming’ kwamba ameita hivyo kwa kuwa anarudi nyumbani lakini pia anaamini mcheza kwao hutunzwa.

Amesema mwitikio mkubwa wa nyumbani ndiyo utawashtua wengi ambao hawamjui na wanataka kumfahamu.

Zuchu amsema kwenye tamasha hilo atapenda kushiriki na wasanii asilimia kubwa wanaotokea Zanzibar kwa kuwa wana uwezo na haki ya kushiriki katika tamasha hilo.

“Nimeongea nao na wameonyesha ushirikiano mkubwa sana, siku hiyo itapambwa na ngoma, benbati, vidumbaki, taarabu za zamani na za sasa lakini pia Zenj fleva ya zamani na sasa.

“Tutakuwa na wasanii wenzangu kutoka Bara ambao mnawajua, nia na dhumuni kubwa ni kushirikiana na wenzangu naamini hakuna cha mmoja kinachofanikiwa kwa ukubwa cha wengi kinafanikiwa kwa ukubwa,” amesema mrembo.

Zuchu amesema tamasha hilo likawe chachu ya maendeleo kwa Zanzibar kitalii, kisanaa, kiukuaji wa biashara, ikainue hamasa kwa wasanii wa Zanzibar.

Pia amesema Julai 24 kutakua na semina kwa wasanii kujifunza mambo mbalimbali ya tasnia jinsi gani wanatakiwa kutumia mitandao ya kijamii kuwaingizia kipato, semina itakayotolewa na wataalamu wa masuala ya sanaa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,283FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles