Zuchu awashukuru mashabiki kwa mapokezi

0
487

NA BEATRICE KAIZA

NYOTA wa muziki wa bongo fleva, Zuhura Omary ‘Zuchu’ amewashukuru mashabiki zake kwa kuupokea wimbo wake mpya aliomshirikisha Diamond Platnumz, uitwao ‘Litawachoma’.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Zuchu alisema hadi sasa hana cha kuwalipa mashabiki zake, lakini anawashukuru kwa mapokezi makubwa.

“Asante mashabiki zangu kwa mapokezi haya, hadi sasa huko Youtube tuna-trend, tuko namba mbili, litawachoma ndani ya saa 15 tu baada ya kuitoa tumefikisha watazamaji zaidi ya laki 5,’’ alisema Zuchu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here