30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 16, 2024

Contact us: [email protected]

Ziwekwe Sheria kali kudhibiti ukatili-World Vision

Shirika la World Vision Tanzania limsema kuwa ili kuweza kupambana na vitendo vya ukatili hasa kwa wanawawake na watoto lazima zitungwe sheria kali.

Mbali na sheria, msisitizo mkubwa unatakiwa kuwekwa katika ufuatiliaji wa matukio ya ukatili wa kijinsia kwenye jamii, ikiwamo kutoa elimu kwa kiwango kikubwa.

Hayo yameelezwa Desemba 10, 2022 na Mratibu wa Shirika hilo kupitia mradi wa Shishiyu ulioko wilayani Maswa Mkoa wa Simiyu, Betty Isaack wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili yaliyofanyika katika kijiji cha Jija wilayani humo.

Amesema jamii katika wilayani humo haina mwamko juu ya masuala ya ulinzi wa mtoto na usawa wa kijinsia kutokana na uwepo wa mila kandamizi dhidi ya wanawake na watoto.

Aidha, ameiomba Serikali kuweka msisitizo mkubwa kwa kufuatilia, kutoa elimu, kuweka mikakati na sheria ndogondogo zitakazowabana watu wenye nia na wanaobainika kufanya vitendo vya kikatili dhidi ya watoto, wanawake na wanaume.

“Jamii bado ina mtizamo hasi juu ya jitihada zinazofanywa na wadau katika kuleta usawa wa kijinsia ambapo ni kikwazo kikubwa katika kufikia azma ya kuwa na jamii inayozingatia usawa wa watoto na usawa wa kijinsia.

Baadhi ya wa shule za msingi za Jija na Shihiyu zilziopo wilayani Maswa Mkoani Simiyu, wakiwa na mabango yenye jumbe za kupinga vitendo vya ukatili, wakati wa kilele za maadhimisho ya siku 16 za kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia.

“Ili kukabiliana na changamoto hii, Halmashauri haina budi kuweka sheria ndogogo tena kali ili kuwabana watu wote wanaotenda matukio hayo, hii itasaidia sana matukio kukoma kwenye jamii zetu,” amesema Betty.

Ofisa Ustawi wa Jamii wilayani humo, Ngais Tarakwa akizungumza kwenye maadhimisho hayo amesema takwmimu zinaoyesha kuwa wanawake wilayani humo wanaongoza katika matukio ya ukatili wa kisaikolojia.

Amesema kutoka Januari hadi Septemba, 2022 wanawake waliofanyiwa ukatili wa kisaikolojia walikuwa 599 huku wanaume wakiwa 162, ukatili wa kimwili wanawake 120 na wanaume 70, kutelekezwa wanawake 63 na wanaume 59, na ukatili wa kingono wanawake 87 na wanaume 8.

“Mwaka 2021 waliofanyiwa ukatili wa kisaikolojia wanawake walikuwa 984 na wanaume 179, ukatili wa kimwili wanawake walikuwa 282 na wanaume 113, kutelekezwa wanawake 230 na wanaume 122, ukatili wa kingono wanawake 98 na wanaume 7,” amesema Tarakwa.

Amewataka akinamama na watoto wa kike kuendelea kutoa taarifa za ukatili wa kijinsia katika mamlaka za serikali na wadau wa maendeleo ikiwemo mashirika yanayopambana na ukatili katika jamii.

Akimwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Ofisa Tarafa ya Shishiyu, Saguda Sayayi aliitaka jamii kuimarisha malezi ya watoto katika familia ikiwemo kuwapatia elimu watoto bila kujali jinsia, umri au hali ya ulemavu.

Amesema mtoto wa kike ana haki ya kupata elimu sawa na mtoto wa kiume na pia mwanamke ana haki sawa ya umiliki mali katika familia sawa na mwanaume na kuitaka jamii kuendelea kutoa taarifa dhidi ya vitendo vya ukatili.

Perpetua Sayayi ambaye ni mwanafunzi kutoka Jija A shule ya msingi aliiomba serikali kuchukua hatua kali dhidi ya vitendo vya ukatili vinavyotokea katika jamii ikiwemo mimba za utotoni zinazokwamisha wasichana kufikia ndoto zao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles