30.4 C
Dar es Salaam
Friday, September 24, 2021

Zitto Kabwe ahukumiwa kifungo cha nje cha mwaka mmoja

KULWA MZEE, DAR ES SALAAM

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemtia hatiani Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe na kumuhukumu kifungo cha nje cha mwaka mmoja kwa sharti la kutotamka wala kuandika kauli za uchochezi mitandaoni baada ya kupatikana na hatia ya makosa matatu ya uchochezi yaliyokuwa yanamkabili.  

Hukumu hiyo imesomwa asububuhi ya leo Ijumaa Mei 29, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi baada ya upande wa mashtaka na utetezi kufunga ushahidi na kuwasilisha majumuisho ya mwisho kwa kuirahisishia mahakama kufikia uamuzi.

Katika kesi hiyo upande wa mashitaka una mashahidi 15 na utetezi ulikuwa na mashaidi nane.

Zitto anadaiwa Oktoba 28, mwaka juzi katika mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika ofisi za Makao Makuu ya ACT Wazalendo aliitisha mkutano na waandishi wa habari akiwa na lengo la kuleta chuki kwa raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kinyume na sheria na kutoa maneno ya uchochezi dhidi ya Jeshi la Polisi.

Hakimu Shaidi amesema upande wa mashtaka katika kesi hiyo umeweza kuthibitisha kosa dhidi ya mshtakiwa bila kuacha shaka yoyote.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
157,854FollowersFollow
518,000SubscribersSubscribe

Latest Articles