24.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 31, 2023

Contact us: [email protected]

Zitto akana mashtaka ya uchochezi mahakamani

 KULWA MZEE, DAR ES SALAAM

MBUNGE wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe amekana kufanya mkutano na waandishi wa habarikuzungumzia mauaji ya wananchi waliouawa Kijiji cha Mpeta Nguruka, Uvinza mkoani Kigoma, maneno yanayodaiwa ni uchochezi.

Zitto alikana jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi wakati akisomewa maelezo ya awali na Wakili wa Serikali,Nassoro Katuga.

Mshtakiwa huyo alikana kwamba Oktoba 28, 2018 katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika ofisi za makao makuu ya Chama cha ACT Wazalendo kwa nia yakuleta chuki  miongoni mwa wananchi waTanzania dhidi ya Jeshi la Polisi, alitoa maneno ya uchochezi.

Alikana maneno ambayo anadaiwa kuyasema kuwa “watu ambao walikuwa ni majeruhi katikatukio la mapambano baina ya wananchi na polisi, wakiwa wamekwenda hospitali kupata matibabu katika Kituo cha Afya cha Nguruka, polisi wakapata taarifa kuwakuna watu wanne wamekwenda hospitali Kituo cha Afya Nguruka kupata matibabu wakawafuata kule wakawaua”.

Katuga alidai maneno hayo yalikuwa ni ya uchochezi, yenye kuleta hisia ya hofu nachuki.

Mshtakiwa anadaiwa kutoa maneno kwamba “lakini tumefuatilia kwa kina jambo hili, taarifa ambazo tumezipata kutoka kijijini Mpeta Nguruka, Uvinza ni mbaya, ni taarifa ambazo zinaonesha wananchi wengi sana wameuawa na Jeshi la Polisi, pamoja na kwamba Afande Sirro wamekwenda kule, halijatoa taarifa yoyote kuhusu wananchi… kama hawa Wanyantuzu walivamia eneo la ranchi, kuna taratibu za kisheria za kuchukua na siyo kuwaua, wananchi wengi sana wamekufa”.

Katuga alidai Zitto katika mkutano huo huo alitoa waraka kwa umma ukiwa na maneno yakichochezi kwa nia ya kuleta chuki kwa Watanzania dhidi ya polisi.

Pia Zitto anadaiwa alitoa maneno “Tumekuwa tukifuatilia kwa kina yanayojiri yote huko Uvinza… tunasikitika kusema kuwa taarifa tunazozipata kutoka Uvinza zinaogofya mno, kwani tunaambiwa kuwa wananchi zaidi ya 100 wa kabila la Wanyantuzu wamepoteza maisha kwa kupigwa risasi na polisi, wengine wakisemwa kuuawa hatawakiwa kwenye matibabu hospitalini baada ya kujeruhiwa kwenye purukushani na Jeshi la Polisi”.

Zitto alikana kutamka maneno hayo yote, lakini alikubali kwamba alikamatwa Novemba 30 nyumbani kwake Masaki, Dar es Salaam na kufikishwa Kisutu kwa mara yakwanza,  Novemba 2 mwaka huu kujibu mashtaka.

Wakili Katuga alimaliza kusoma maelezo hayo kisha akaomba mahakama impe muda kuanda amashahidi na kesi hiyo imeahirishwa hadi Januari 14 mwakani kwa kutajwa na Januari 29 kuanza kusikiliza mashahidi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,208FollowersFollow
567,000SubscribersSubscribe

Latest Articles