25.2 C
Dar es Salaam
Sunday, December 1, 2024

Contact us: [email protected]

ZIMBABWE WAPELEKA WANAWAKE BRAZIL KUTAFUTA KIZAZI CHA SOKA

BADI MCHOMOLO NA MITANDAO


Zimbabwe-National-TeamKILA nchi imekuwa na mipango yake tofauti katika kuhakikisha inafanya vizuri kwenye soka la kimataifa ili kuweza kuitangaza nchi kwa ujumla.

Kwa nchi ambazo zimeendelea zinakuwa na shule za kufundisha soka kwa vijana wadogo sana, ili wakiwa wakubwa waweze kutoa mchango wao.

Mbali na kuwa na shule hizo, wengine wanaamua kuwekeza fedha nyingi kama vile kununua wachezaji wenye majina makubwa ili kuleta chachu kwa wachezaji wa nchi husika.

Nchini China, wameamua kuwekeza kwa kiasi kikubwa katika soka, huku wakidai kuwa hadi kufikia 2020 nchi hiyo itambulike katika ulimwengu wa soka.

Baadhi ya mipango yao ni kwamba, kila eneo lenye watu kuanzia 10,000 lazima pawe na viwanja vya soka si chini ya 20 ili vijana wengi wapate nafasi ya kujifunza soka, hata hivyo inasemekana wamepeleka vijana wadogo katika klabu ya Real Madrid na Barcelona nchini Hispania kwenda kujifunza soka ili wakirudi wawe wameiva kulisaidia taifa lao.

SPOTIKIKI leo hii imekuandalia maandalizi ambayo yanafanywa na Taifa la Zimbabwe kwa ajili ya kuja kuwa na kizazi cha soka baadaye.

Zimbabwe wamekuwa tofauti kidogo na mataifa mengine ambapo nchi hiyo inaamini kuwa soka lipo nchini Brazil ambako kuna vipaji vya hali ya juu.

Kutokana na hali hiyo, Serikali ya nchini Zimbabwe imeamua kupeleka wanawake 10 nchini Brazil, wanawake hao wanacheza soka nchini humo ili wakapewe ujauzito na wachezaji wa zamani wa Brazil kwa ajili ya kupata mbegu ambayo itatoa kizazi cha soka.

Vyombo vya habari nchini Brazil vimethibitisha kuwa Kusini mwa Afrika kuna tatizo la wachezaji wenye vipaji vikubwa kama ilivyo barani Ulaya, labda kuwe na mbegu za wachezaji wa zamani.

Serikali hiyo ya Zimbabwe ilianza kufikia makubaliano na nchini Brazil tangu mwaka 2010 baada ya timu ya taifa ya Brazil kucheza mchezo wa kirafiki na Zimbabwe kwenye uwanja wa Zimbabwe National Sports, ambapo makubaliano hayo yalijadiliwa na Rais wa Shirikisho la Soka nchini humo, Phillip Chiyangwa.

Brazil ilicheza na timu hiyo ambapo walikuwa wanajiandaa na michuano ya Kombe la Dunia ambayo ilifanyika nchini Afrika Kusini.

Wanaamini kwa kufanya hivyo watafanikiwa kupata watoto ambao watakuwa na kizazi cha soka kwa miaka ya baadaye na Zimbabwe kuja kuwa hatari katika soka kama yalivyo mataifa mengine.

“Tunajivunia kwa wanawake 10 wa nchini Zimbabwe kujitoa muhanga na kukubali kwenda nchini Brazil kupigania taifa lao la baadaye katika soka, mpango huo unajulikana kwa jina la NSGF.

“Madaktari wa nchini Zimbabwe wamekubaliana na wale wa nchini Brazil kwa kutaka kufanya mpango huo kuona uwezekano wa kupata mbegu za nyota hao wa zamani wa soka ambao wamestaafu kwa ajili ya kizazi chao kukiendeleza nchini Zimbabwe.

“Tayari majaribio ya kupata mbegu za nyota hao yamefanyika na tunatarajia kuona majibu mazuri hivi karibuni,” alisema msemaji wa shirikisho hilo.

Katika wanawake hao ambao wamekwenda nchini Brazil baadhi yao bao wanacheza soka ambao ni wanane, huku wawili wakiwa wamestaafu, kati ya wanane hao watano wapo katika sehemu ya timu ya taifa ya nchini Zimbabwe.

Wakati huo wanawake watatu wakiwa wanacheza ligi ya wanawake daraja la kwanza nchini Zimbabwe.

Mfumo huo Zimbabwe wanaamini kuwa unaweza ukawasaidia kuwa na kizazi cha wachezaji wenye uwezo mkubwa kwa miaka ya baadaye ambao wataweza kushindana duniani.

Huu ni mpango ambao wameuangalia kuanzia miaka 20 ijayo, si lazima wazaliwe watoto wa kiume pekee hata wakiwa na wakike wanaamini wataendelea kuwa na chembechembe za soka la Brazil.

Endapo watapatikana watoto wa kike, basi wanaamini watoto hao watakuja kupata watoto katika maisha yao ambapo wanaweza kuwa wa kiume huku bado wakiwa na chembechembe hizo.

Huo ni mpango mpya kwa nchi za Afrika ambao unatazamiwa matunda yake kwa muda mrefu ujao, hapo panatakiwa kuwa na uvumilivu kwa kuwa ni muda mrefu tofauti na mipango ya China ambayo ndani ya miaka mitano kuanzia sasa mabadiliko makubwa yataonekana katika soka lao.

Zimbabwe wanachokiangalia ni kuja kushiriki michuano mikubwa kama vile Kombe la Dunia na ikiwezekana kuja kulichukua na kulileta barani Afrika.

Lakini Afrika ikiwa inapangwa mipango kama hiyo ambayo inaonekana ni dhaifu kuliko ile ya mabara ya Ulaya ni wazi kwamba ni safari ndefu kuweza kuwafikia kutokana na uwekezaji wao.

Inawezekana mipango hiyo ya Zimbabwe ikaja kuleta ushindani kwa soka la Afrika, kwa kuwa kwa bara la Ulaya watakuwa wamezidi kusonga mbele zaidi kwa kuwa ndio maisha yao ya kila siku na wanazidi kushindana kutokana na utajiri wao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles