24.4 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

Zimamoto wahamasishwa kujiunga Saccos

Na  Sheila Katikula, Mwanza

Kamishna Jenerali  wa Jeshi la Zimamoto  na Uokoaji Tanzania, John Masunga amewahamasisha watumishi wa jeshi hilo kujiunga na  Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo cha  zimamoto Sacco’s ili waweze kupata kujiwekea akiba na kupata mikopo ya kutimiza malengo yao.

Masunga alitoa wito huo jana wakati wa mkutano mkuu wa pili wa mwaka  wa zimamoto sacco’s uliofanyika jijini Mwanza wenye lengo la kuhamasisha watumishi wa Jeshi hilo kujiunga na kununua hisa za Zimamoto Sacco’s limited. 

Masunga ambae alikuwa mgeni rasmi kwenye mkutano huo alisema ni vema watumishi hao  kujiunga na mfuko huo ili uweze kuwahudumia na kukidhi mahitaji yao pindi watakapo hitaji huduma kutoka kwenye Sacco’s hiyo. 

“Kauli mbiu inasema Ushirika suluhisho la mtaji, nawaomba muendelee kuwahamasisha watumishi wengine ambao hawajajiunga na Sacco’s hii wachangamkie fursa ili waweze kununua hisa,” alisema Masunga.

Alisema ingawa Sacco’s hiyo ni changa kwa kuwa ilianza mwaka 2019 lakini hadi sasa imeanza vizuri na imepata mwitikio wa kutosha kutoka kwa wanachama waliokwisha jiunga na mfuko huo. 

Alisema  uwepo wa Sacco’s hiyo utawasaidia watumishi hao kupata mikopo kwa riba nafuu ukilinganisha na Taasisi nyingine za kifedha.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa bodi hiyo, Christina Sunga alisema Sacco’s hiyo ilianzishwa kwa lengo la  kusaidia kukuza uchumi katika jamii ya jeshi hilo. 

Alisema Sacco’s hiyo inawanachama 207 miongoni mwao waliolipa hisa ni 124 huku 83 wakiwa bado hawajalipa hisa zao na kuongeza kuwa zinazotolewa ni upokeaji na utunzaji wa hisa akiba utoaji wa mikopo mbalimbali ikiwamo  mikopo ya elimu ya juu wa dharula na maalum ambayo  riba yake ni asilimia mbili.

Naye mwanachama wa zimamoto Sacco’s ambaye ni Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi hilo kutoka Mtwara Bilhah Chailla ametunukiwa cheti baada ya kukidhi vigezo vya kununua hisa 10 ambazo ni sehemu ya umiliki wa mtaji  wa chama.

Insipekta Hamisi Dawa ni mwanachama wa sacco’s hiyo kutoka Kagera amewaomba wanachama wenzake kumaridhia michango yao ili waweze kulipia hisa na kupelekea kunufaika na mikopo ya mfuko huo. 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles