23.6 C
Dar es Salaam
Wednesday, September 27, 2023

Contact us: [email protected]

Ziara za Rais Samia zawanufaisha Wafanyabiashara Buguruni

Na Hadia Khamis, Mtanzania Digital

Ziara za Rais Samia Suluhu Hasan zimezidi kuwanufaisha Wafanyabiashara nchini ikiwamo ongezeko la bidhaa ikilinganishwa na kipindi cha nyuma.

Hayo yamebainishwa na Meneja wa Soko la Matunda la Buguruni jijini Dar es Salaam Selemani Mfinanga wakati akizungumza na Mtanzania Digital sokoni hapo.

Amesema ziara za Rais Samia nje ya nchi zimesaidia kwa kiasi kikubwa ongezeko la bidhaa za matunda sokoni hapo.

“Kuondoshwa kwa vikwazo vya kibiashara baina ya nchi ya Kenya na Tanzania sisi wafanyabiashara kumetusaidia kwa kiwango kikubwa.

“Kwa mwaka wa fedha 2022/2023 tunatarajia kukusanya mapato kwa njia ya kumbukumbu namba ili kuweka usalama wa fedha. Mfumo huu tayari tunautumia ila hadi kufikia 2023 utakuwa unatumika kwa asilimia 100,” amesema Mfinanga.

Ameongeza kuwa asilimia 80 ya mazao yanayoingizwa katika soko hilo
yanategemea soko la ndani na asilimia 20 ni kutoka soko la nje kwenye nchi za Kenya na nyingine.

Ameongeza kuwa kwa sasa bado soko hilo linakabiliwa na ufinyu wa eneo kwani baadhi ya wafanyabiashara wanapanga juani bidhaa zao.

Alisema mpango wa Serikali kwa sasa ni kutengeneza masoko ya kisasa na ya muda mrefu ili kuondokana na changamoto hizo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,729FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles