23.6 C
Dar es Salaam
Wednesday, September 27, 2023

Contact us: [email protected]

Ziara ya Waziri Mkuu Mwanza hofu tupu

Kassim MajaliwaNa Benjamin Masese, Mwanza

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa leo anatarajiwa kutua jijini Mwanza kwa ziara ya siku 14 katika mikoa mitatu ya Kanda ya Ziwa, huku kukiwapo na hofu kubwa kwa viongozi wa Serikali na mashirika ya umma kutumbuliwa majipu.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo, alisema Majaliwa anatarajiwa kuwasili Mwanza leo mchana na kupokewa na viongozi mbalimbali wa Serikali.

Alisema baada ya kuwasili, kesho ataelekea mkoani Simiyu kutembelea shughuli mbalimbali za maendeleo.

“Tunaomba kuwataarifu wananchi wa Mkoa wa Mwanza kuwa tutakuwa na ugeni mzito wa viongozi wawili wa kitaifa ndani ya mkoa wetu kwa nyakati tofauti, kwanza tunatarajiwa kesho (leo) kumpokea Waziri Mkuu Majaliwa na kuwa naye siku moja hapa. Hatakuwa na ziara, lakini ni uamuzi wake pengine anaweza kufika na kutaka kutembelea sehemu yoyote atakayoamua.

“Ila sisi kama mkoa tunampokea kwa sababu anatumia Uwanja wa Ndege wa Mwanza na kupumzika hapa Ikulu ndogo na baadaye Machi 2 ataanza ziara yake katika Wilaya ya Busega mkoani Simiyu na wilaya nyingine za mkoa huo kabla ya kwenda Geita na Kagera. Ziara yake Kanda ya Ziwa itakuwa ya siku 14…tutampokea tana hapa Mwanza Machi 14 wakati akirejea kwenda mkoani Dodoma.

“Hivyo tunawaomba wananchi wajitokeze kwa wingi kuanzia  pale uwanja wa ndege, ambapo atapata fursa ya kuzungumza nao kadiri itakavyokuwa, kwa wale watumiaji wa barabara ya uwanja huo itafungwa kuanzia mchana hadi atakapopita na kufika Ikulu ndogo,” alisema.

Ujio wa Majaliwa umekuwa gumzo mkoani hapa kwa kuleta hofu kwa watendaji wa Serikali na kampuni za umma kutokana na rekodi yake ya kufanya ziara ya kushtukiza na kutumbua majipu.

Wakati huo huo, Janeth Magufuli, mke wa Rais Dk. John Magufuli, naye anatarajiwa kuwasili mkoani Mwanza  Machi 4.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,729FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles