27.1 C
Dar es Salaam
Thursday, December 7, 2023

Contact us: [email protected]

Ziara ya Papa Msumbiji yazua gumzo

MAPUTO, MSUMBIJI

SERIKALI ya Msumbiji inatarajia kutumia karibu Dola za Marekani 325,000 (£266,000)  sawa na shilingi za Tanzania takribani milioni 750 kwa ajili ya maandalizi ya ziara ya Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis wiki ijayo.

Redio ya serikali ndiyo iliyotangaa kiwango hicho cha fedha na kueleza kuwa kila mmoja ameonekana kufurahia.

” Kuna bajeti ya msingi, lakini inarekebishwa, ukizingatia kuwa wakati mambo kama haya yanafanywa, kuna hali fulani ambazo zinahitaji kushughulikiwa,” Waziri wa Mambo ya Nje, Jose Pacheco aliiambia Redio Msumbiji, akithibitisha kiwango hicho.

Baadhi ya wakazi katika jiji la Maputo waliliambia Shirika la Utangazaji la Uingereza la BBC kuwa kiwango hicho cha fedha kinapaswa kutumika kuboresha jiji haijalishi ni mtu gani muhimu anatembelea.

“Huu ni ujinga! Kwanini tusubiri hadi ziara ya Papa ndipo tuufanye mji wetu uwe mzuri? Hivi ndivyo Maputo inavyopaswa kuonekana wakati wote,” alisema Bernicia Cotela akielezea jinsi maandalizi ya kuuweka sawa mji wa Maputo kwa ajili ya ziara hiyo ya Papa yalivyoshika kasi.

“Ni kama kupaka kipodozi kwenye mwili wako kabla ya kuoga. Kwanini uchore picha nzuri katika kitu ambacho sio cha kweli?”

Wengine, kama Afonso Silveira, anadhani kiwango kilichotangazwa kwa ajili ya maandalizi hayo ni sahihi kwa sababu kuhakikisha ulinzi wa Papa ni jambo linalohitaji uwekezaji mkubwa … ikiwa ni pamoja na barabara, kanisa na viwanja.

” Lakini pia nina maoni kama suala la usafi, ulinzi na ukarabati wa jiji ni lazima iwe kazi ya kudumu kwetu sote, pamoja na serikali,” aliongeza

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
580,000SubscribersSubscribe

Latest Articles