31.8 C
Dar es Salaam
Tuesday, January 31, 2023

Contact us: [email protected]

Zesco, Zanaco kujifunza kwa Azam

azamfcNA ADAM MKWEPU, DAR ES SALAAM

KLABU ya soka ya Azam FC imeendelea kujiongezea umaarufu na kutengeneza jina lake kimataifa kwa kuzivutia klabu za Zesco United na Zanaco (Zambia) pamoja na Mabingwa wa Zimbabwe, Chicken Inn kuwa na dhamira ya kuja kujifunza soka la Tanzania.

Akithibitisha ukweli wa jambo hilo jana, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Saad Kawemba, alisema timu zote tatu zimeonyesha nia ya kuja Tanzania kucheza pamoja na kujifunza namna Azam inavyoendesha timu yao.

“Tunawashukuru waandaaji wa michuano hiyo kwa kutupa nafasi na tumeona kuwa klabu yetu ina heshima, sasa hivi watu wanaiheshimu na wanaona kabisa kuna kitu tofauti cha kujifunza kutoka Azam FC tofauti na ilivyokuwa huko nyuma.

“Klabu zote zinazoshiriki michuano hii kwa ufasaha kabisa zimeonyesha dhamira ya kuja Dar es Salaam kucheza na sisi na kuja kujifunza tunachokifanya, tunaendeshaje mpira na tuna kitu gani Azam FC.

“Tumewapa nafasi hiyo ya kuja Dar es Salaam, kwa hiyo tutegemee klabu kama Zesco itakapokuwa inakwenda kucheza Sudan Kusini kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika (AL Ghazala Wau FC), wanaweza kuweka kambi Dar es Salaam, pia tunatarajia ujio wa Chicken Inn pamoja na Zanaco,” alisema.

Kawemba alifungua milango kwa klabu nyingine yoyote ambayo inapenda kujifunza kupitia Azam FC na kudai kuwa, ni muda wa kushirikiana na klabu kutoka nje ili kubadilishana uzoefu.

“Hatushangai kuona klabu za nyumbani haziwezi kujifunza kupitia kwetu, lakini muda utafika na wataona umuhimu wa kuja kujifunza,” alisema.

Azam FC ipo kileleni kwenye michuano hiyo kwa pointi nne sawa na Zanaco, hii ni baada ya kutoa sare ya bao 1-1 dhidi ya Zesco United katika mchezo wa ufunguzi kabla ya kuichapa Chicken Inn mabao 3-1.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,063FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles