29.9 C
Dar es Salaam
Sunday, November 17, 2024

Contact us: [email protected]

Zege halilali, Rais Samia atangaza baraza la mawaziri

Na Faraja Masinde, Dar es Salaam

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Saia Suluhu Hssan, leo Jumatano Machi 31, 2021 amefanya uteuzi wa Mawaziri na Naibu Mawaziri huku akifanya mabadiliko madogo kwa kuwahamisha baadhi ya mawaziri.

Aidha, Rais Samia aimeihamisha Ofisi ya Waziri Mkuu kutoka ofisi ya Rais, Wizara ya Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji.

Aidha, Rais Samia amefanya uteuzi wa wabunge watatau ambao ni Balozi Dk. Bashiru Ali Kakurwa kuwa mbunge ambaye aliwa alikuwa Katibu Mkuu Kiongozi.

Mbali na Dk. Bashiru, wengine walioteuliwa kuwa wabunge ni Balozi Liberata Mulamula kuwa mbunge na Balozi Mbaruku Nassoro Mabaruku kuwa mbunge.

Walioteuliwa kuwa Mawaziri:

  • Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa – Elias Kwandikwa
  • Utumishi na Utawala Bora- Mohamed Mchengelwa (Kapten (Mst.) John Mkuchika)- amepangiwa kazi maalumu Ofisi ya Rais
  • Wizara ya Ardhi- William Lukuvi
  • Wizara ya Maji- Juma Aweso
  • Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo- Innocent Bashungwa
  • Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Wenye Ulemavu –  Jenista Mhagama
  • Wizara ya Fedha na Mipango- Dk. Mwigulu Nchemba
  • Wizara ya Mambo ya Nje- Balozi Liberata Mulamula
  • Wizara ya Afya- Dk. Dorothy Gwajima
  • Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji- Geofrey Mwambe
  • Wizara ya Katiba na Sheria – Prof. Paramagamba Kabudi
  • Wizara ya Elimu- Prof. Joyce Ndalichako
  • Wizara ya Mifugo na Uvuvi – Mashimba Ndaki
  • Wizara ya Maliasili na Utalii – Dk. Damas Ndumbaro
  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa – Ummy Mwalimu
  • Wizara ya Nishati- Dk. Medard Kalemani
  • Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi- Dk. Leonard Chamuriho
  • Wizara ya Kilimo- Prof. Adolf Mkenda
  • Wizara ya Madini- Doto Biteko
  • Wizara ya Viwanda na Biashara- Prof. Kitila Mkumbo
  • Wizara ya Mambo ya Ndani- George Simbachawene
  • Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira)- Seleman Jafo
  • Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari- Dk. Faustine Ndugulile

Naibu Mawaziri:

  • Wizara ya Viwanda na Biashara- Kigae Silaoneka
  • Wizara wa Ardhi- Angelina Mabula
  • Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira- Patrobas Katambi
  • Wizara ya Mambo ya Ndani- Hamis Hamza Hamisi
  • Wizara ya Fedha- Hammad Masauni
  • Wizara ya Elimu- Kipanga Juma Omar
  • Ofisi ya Rais TAMISEMI – Dk. Festo Ndugange
  • Wizara ya Nishati- Stephen Byabato
  • Menejimenti Utumishi wa Umma- John Ndejembi
  • Mawasiliano na Teknolojia ya Habari- Pauline Gekul
  • Wizara ya Mifugo- Abdallah Ulega
  • Wizara ya Madini- Ndulane Kumba
  • Wizara ya Ujenzi- Godfrey Kasekenya
  • Ofisi ya Waziri Mkuu wenye ulemavu- Ummy Ndelinanga
  • Wizara ya Maji- Maryprisca Mahundi
  • Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo-
  • Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira)- Hamadi Hassan Chande
  • Wizara ya Mambo ya Nje- Mbarouk Nassor Mbarouk
  • Wizara ya Maliasili na Utalii- Mary Masanja
  • Ofisi ya Rais TAMISEMI- David Silinde
  • Wizara ya Kilimo- Hussein Bashe
  • Wizara ya Afya- Dk. Godwin Mollel na Mwanaidi Ally Khamis
  • Wizara ya Katiba na Sheria- Pinda Mizengo
  • Wizara ya Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji- William Ole Nasha
  • Wizara ya Viwanda na Biahsra- Exaud Kigae
- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles