Zawadi NT aichambua ‘Glory’

0
293

QUEENSLAND, AUSTRALIA

MWIMBAJI anayekuja kwa kasi kwenye muziki wa Injili kutoka Australia, Zawadi NT, ameweka wazi kuwa wimbo wake mpya, Glory, umebeba ujumbe mzuri wa kumshukuru na kumtukuza Mungu.


Zawadi mwenye asili ya Jamhuri ya Kidemoksraia ya Kongo (DRC), ameliambia MTANZANIA kuwa wimbo huo ni wa kwanza tangu alipoanza kufanya huduma hiyo hivyo anahitaji kupata mashabiki wapya kutoka Tanzania.


“Wimbo una siku chache kwenye chaneli yangu ya YouTube lakini nimeona mapokezi mazuri japo bado nahitaji kuwafikia wengi. Glory ni wimbo wa kusifu na kumwabudu Mungu kwahiyo kila mtu anaweza kuusikiliza na kubarikiwa nao,” alisema Zawadi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here