27.9 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Zari aongoza mastaa kutema cheche sakata la Shilole

 CHRISTOPHER MSEKENA 

UKATILI wa wanawake na watoto ni miongoni mwa changamoto kubwa zilizopo kwenye jamii nyingi za Waafrika ambazo zinaamini kwamba mwanamke ni kiumbe dhaifu. 

Tumeshuhudia wanawake kadhaa wakipoteza maisha kwa vipigo kutoka kwa waume zao huku wengine wakibaki walemavu na majereha ya kudumu kwenye miili na hata katika afya zao za akili. 

Kutoka Afrika Kusini mama watoto wa Diamond Platnumz, Zari The Boss Lady, ameweka wazi kwamba na yeye ni miongoni mwa waathirika wa unyanyasaji huo kutoka kwa aliyekuwa mumewe. 

Hatua hiyo imekuja baada ya msanii wa Bongo Fleva na mjasiliamali, Zuwena Mohamed ‘Shilole’, kuvunja ndoa yake na Ashrafu Sadiki maarufu kama Uchebe kwa madai ya kunyanyaswa kwa vipigo, dharau na usaliti. 

Kwa kutumia ukurasa wake wa picha, Zari The Boss Lady aliweka wazi kuwa chanzo cha kuondoka kwenye ndoa  yake na Ivan licha ya utajiri mkubwa ni unyanyasaji wa kipigo. 

“Mara nyingi nimekuwa nikiulizwa kwa nini naacha utajiri wote wakati wanawake wengine wanautafuta. Niliitwa mjinga huku wakiwa hawajui kitu ambacho kipo nyuma ya pazia mimi ni muhanga wa unyanyasaji wa kimwili, ilichukua ujasiri mkubwa sana wa kuweza kujitambua na kusema kwa sasa inatosha,” anasema Zari. 

Aliongeza kuwa wanawake wengi maarufu huwa wanaogopa kuongea kama Shilole kuhusu unyanyasaji wanaofanyiwa na wapenzi wao kwa sababu ya hofu watu watachukuliaje. 

“Mtu anaweza mimi mtu maarufu itaniletea aibu kwenye jina langu, sina sehemu ya kwenda, wapi nitakula, siwezi kupata kazi, nawaondoa watoto wangu kwa baba yao, nitakataliwa na familia yangu, nitakuwa mke au mwenza mbaya kwa sababu baadhi ya wanawake wa kiafrika walikuzwa katika katika mazingira ya kubaki na waume zao kwa vyovyote itakavyokuwa,” anasema. 

Zari aliongeza kuwa miongoni mwa mbinu zinazotumiwa na polisi wa Afrika Kusini kukomesha wanaume wanaonyanyasa wanawake na watoto ni kuwaweka kwenye lupango moja na watu waliodata na vifungo vya maisha ili wakomeshwe. 

“Polisi aliniambia wao huwa wanawaweka mahabusu wanaume wanaopiga wanawake pamoja na wafungwa wanaotumikia kifungo cha maisha ambapo wafungwa wanaotumikia kifungo cha maisha wanawanyanyasa hao wanaume ili kuwaonjesha ladha ya unyanyasaji ipoje kwa sababu huwezi ijua ladha ya shubiri mpaka uonje,” anasema. 

Mastaa kadhaa wametema cheche zifuatazo kuhusiana na sakata la Shilole kupigwa na mumewe ambaye kwa utetezi wake alisema, picha alizoweka mkewe mtandaoni ni za zamani na ana muda mrefu hajampiga. 

Flaviana Matata: “Haijalishi mwanamke kafanya nini huruhusiwi kumpiga, hakuna kitu 

kinacho halalisha hii, natumaini kuna kitu kitafanyika ili na wengine wajifunze.” 

Rosa Ree: “Shilole ni mwanamke mzuri, mrembo, mwenye akili na mpambanaji, mwanaume yeyote anatakiwa kujua kwamba ana bahati kubwa sana hata kuwepo katika chumba kimoja na wewe, haustahili mwanaume asiyejua thamani yako.” 

Nikki Mbishi: “Tusijaji hili suala kwa mtazamo wa upande mmoja mimi nasimama na Uchebe, samahani wanawake sina maana kwamba naunga mkono wanaume wanaopiga wake zao ila amekandamizwa sana kwa sababu alichokifanya yeye kimeonekana. 

“Nasimama na Uchebe kwa sababu na yeye ni binadamu nishasema kisasi hakijui mpaka, ukinipiga konzi mimi nakukata na panga harafu nitajuta baadaye kwahiyo na Uchebe asikilizwe harafu nyale ni mambo ya ndani sana mpaka yamefika mtandaoni, mimi sijawahi kuona baba yangu na mama yangu wanachoreshana vile kwenye mitandao.” 

Ruby: “Shilole simama usiyumbe usikate tamaa usichoke, usipoteza uelekeo kwenye maisha yako simama imara, naamini wewe ni shujaa ulipotoka na ulipo ni Mungu na hata unapoelekea atabaki kuwa Mungu.” 

Nuh Mziwanda: “Hili jambo kuliongelea nilikuwa sitaki lakini nimeona linakuja sana kwangu, nimelikimbia hadi sasa naona linazidi, nikiwa kama baba mwenye mtoto wa kike na mwanangu anaweza kuja kupata mume na akifanyiwa kitendo kama hicho sitaweza kuvumilia.” 

Madee: “Uchebe umetudhalilisha wanaume, mwanamke hapigwi kama kishandu hata kama umemfumania.” 

Waziri Hamisi Kigwangalla: “Hakuna kosa linaloweza kuhalalisha kipigo kwa mkeo cha namna hii, labda kama utuambie kwamba aliyetoa kipigo hiki ana aina mojawapo ya ugonjwa wa akili na amesahau kunywa dawa zake siku hiyo. Si vingine, wanaume tuna wajibu wa kuwapenda, kuwahurumia na kuwahudumia wake zetu.” 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles