27.5 C
Dar es Salaam
Sunday, December 3, 2023

Contact us: [email protected]

Zari agawa taulo za kike kwa wanafunzi Mwanza

Na Sheila Katikula, Mwanza

Kuelekea siku ya Maadhimisho ya Hedhi Duniani Mei 28, mwaka huu, kampuni ya Doweicare Technology Limited ya imetoa msaada wa taulo za kike aina ya Soft Care zenye thamani ya Sh milioni 13 kwa wanafunzi wa kike 10,008 wa shule mbalimbali za wilayani Misungwi mkoani Mwanza.

Akizungimza kwenye hafla ya kugawa taulo hizo, Balozi wa kampuni hiyo Zarina Hassan maarufu kama “Zari the Boss Lady” amesema msaada huo umetolewa kwenye shule za sekondari 32 na shule za msingi 150 ili waweze kujiamini pindi wanapokuwa katika hedhi.

Hata hivyo amewataka wazazi na walezi kuona umuhimu wa kununua taulo za kike pindi wanapofanya mahitaji ya watoto wao ya shule.

“Nawaomba wazazi na walezi mtambue umuhimu wa kununua taulo za kike kwa watoto wenu na siyo kuwaacha watumie vitambaa wakati wa hedhi kwa sababu ukivaa muda mrefu hutoa halufu mbaya na kusababisha kukosa raha kwa watu na kubabisha kushindwa kusoma,” amesema Zarina.

Hata, hivyo ameiomba kampuni ya Dowecare kuanzisha kampeni ya kutoa msaada wa taulo za kike kwa watoto wa kike nchi nzima.

Nae, Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Victor Zangh amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa jitihada za kuweka mazingira bora kwa wawekezaji na kupelekea zaidi ya Watanzania 2000 kupata ajira kwenye kampuni hiyo.

Amesema siyo mara kwanza kutoa msaada huo kwa jamii kwani kampuni hiyo inatambua msaada unaanzia nyumbani.

Kwa upande wake Mwanafunzi wa shule ya misungwi sekondari, Sabrina Yahaya akisoma risala kwa niaba ya wanafunzi wenzake amesema kutumia tailo za kike kuna faida kwani humfanya msichana kuwa na amani wakati wa hedhi na kuwa msafi muda wote na kuwa huru.

“Kutumia vitaamba wakati wa hedhi kuna changamoto mbalimbali ikiwemo kupata michubuko, kupata miwasho,”amesema Sabrina.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhanidisi Robert Gabriel ambaye alikuwa mgeni rasmi ameishukuru taasisi hiyo kwa kutoa msaada huo kwenye shule mbalimbali zikiwemo za sekondari na msingi za Imee, Igokelo, Eplase, Jitihada, Zulu, Misungwi, Mirembe hata hivyo ameziomba taasisi nyingine kuiga mfano wa kampuni hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
579,000SubscribersSubscribe

Latest Articles