27 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

ZANZIBAR YAILIPA TANESCO BILIONI 10/- 

Na Mwandishi Wetu-DAR ES SALAAM


RAIS Dk. John Magufuli, amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,  Dk. Ali Mohamed Shein, Ikulu Jijini Dar es Salaam, ambapo pamoja na mambo mengine walizungumzia hatua ya visiwa hivyo kuhusu sakata la deni la umeme.

Kutokana na hali hiyo tayari Serikali ya Mapinduzi Zanzibar  imeanza kulipa kiasi cha Sh bilioni 10 na itaendelea kulipa deni hilo mpaka litakapomalizika kwa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco).

Taarifa iliyotolewa jana na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu, ilielza kwamba mazungumzo hayo yalihudhuriwa na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO),  Mhandisi Kahitwa Bishaija na Meneja Mwandamizi wa Fedha wa shirika hilo, Sadock Mugendi.

Wakati hayo yakieendelea Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo amewatoa hofu wananchi wa Zanzibar kuwa hawatakatiwa umeme baada ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) kuanza kulipa deni inalodaiwa na TANESCO.

Alisema SMZ imeanza kulipa kiasi cha Sh bilioni 10 na itaendelea kulipa deni hilo mpaka litakapomalizika.

Prof. Muhongo ametoa wito kwa wadaiwa sugu wote wa TANESCO kulipa madeni yao katika kipindi cha siku tano zilizobaki kwa kuwa wasipolipa watakatiwa umeme. 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles