31.3 C
Dar es Salaam
Thursday, November 28, 2024

Contact us: [email protected]

Zanzibar wafaidika na mbegu ya mpunga iliyoboreshwa kwa teknolojia ya nyuklia

Mwandishi Wetu, Simiyu

Wananchi wa Tanzania Visiwani Zanzibar, wameendelea kufaidika na mchele unaotokana na mbegu ya mpunga aina ya Supa BC iliyoboreshwa kwa teknolojia ya nyuklia kwa kutumia mionzi aina ya Gamma iliyotumika kununurisha mbegu hizo.

Mradi huo ulifadhiliwa na Shirika la Kimataifa la Nguvu za Atomiki (IAEA) na kuratibiwa na Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC),  kwa kushirikiana na Chuo kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) na Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Zanzibar (ZARI) kwa lengo la kuhakikisha mbegu hiyo inaboreshwa na kuwa yenye ubora wa hali ya juu.

Akizungumza katika Maonesho ya Nanenane yanayoendelea katika Viwanja vya  Nyakabindi, wilayani Bariadi, mkoani Simiyu, Mtafiti Msaidizi wa mazao ya kilimo katika Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Zanzibar, Hamza Hamid Hamza amesema mbegu hiyo ina ubora na huzalisha mpunga kwa wingi  ambapo kwa sasa ni chaguo la wakulima na wananchi wengi Visiwani Zanzibar.

Amesema mbegu hiyo ina uwezo wa kuzalisha mpunga hadi kufikia tani saba kwa hekta moja ambapo huchukua  muda wa siku 130 hadi kuvunwa kwake hali ambayo kwa sasa imewahamasisha wakulima wengi kulima aina hiyo ya mpunga visiwani humo.

“Mchele unaotokana na mpunga wa mbegu ya Supa BC ni mzuri, wenye harufu nzuri na wenye ladha tamu kwa walaji na wakulima wengi wanashawishika kupanda mbegu hiyo kwa wingi.

“Mpunga huo una  sifa nyingi ikiwamo urahisi katika kufikicha tofauti na mbegu nyingine nyingi za mpunga zilizozoeleka na mmea wake una urefu wa wastani na usioweza kuanguka hata baada ya kubeba mpunga ukiwa shambani hivyo hupelekea kubaki na mazao yote hadi wakati wa kuvuna pamoja na uwezo wa kutoa machipukizi mengi wakati wa ukuaji wake,” amesema Hamza.

Amesema mbegu hiyo iliyozinduliwa rasmi na Wizara ya Kilimo na Mifugo ya Zanzibar mwaka 2011 na kwamba teknolojia hii ya nyuklia kwa kutumia mionzi ya Gamma ikiendelea kutumika inaweza kuleta mabadiliko makubwa katika sekta ya kilimo hasa katika kutafiti wa mbegu mbali mbali za mazao hapa nchini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles