27.9 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

‘Zanzibar hakuna tena mgonjwa wa corona’

Na KHAMIS SHARIF-ZANZIBAR

WAZIRI wa Afya Zanzibar, Hamad Rashid Mohammed, amesema kwasasa hakuna mgonjwa hata mmoja wa corona kwenye kambi zilizokuwa zimetengwa kwaajili ya kuhudumia watu wenye virusi hivyo.

Hamad alisema hayo alipotembelea jengo la Jeshi la Kujenga Uchumi (JKU) ambalo lilitumika kama kambi ya kulaza wagonjwa wa maradhi ya COVID19.

Alisema hatua ya jesho hilo kutoa jengo lake kwa ajili ya wananchi imeonesha ushirikiano na umahiri kwani mbali ya kuokoa maisha ya wananchi pia imeoneshwa kuguswa kwao na janga hilo.

Alisema corona imepungua Zanzibar baada ya Wizara ya Afya kuona hakuna mgonjwa hata mmoja sasa na Serikali kutoa agizo la kuendelea kwa shughuli za ujenzi wa taifa.

 “Hivi sasa hatuna mgonjwa yoyote katika vituo vyetu, nasisitiza maradhi haya bado yapo na yanaua, lazima tusijisahau tuendelee kuchukua tahadhari kama kawaida, atakae hisi dalili afike kituoni kwa huduma  ” alisema.

Hamadi alisema kwa sasa wamefikia asilimia kubwa ya corona visiwani humo, hivyo wananchi wazingatie zaidi maelekezo yanayotolewa na wataalamu wa afya ili kuyatokomeza kabisa.

Kwa upande wake Mkuu wa Utawala wa Jeshi la Kujenga Uchumi Mtoni, Kanali Mussa Shaame, alimshukuru waziri huyo kwa kuwatoa wasiwasi na kuahidi kumpa ushirikiano katika kupambana na janga hilo.

“Sisi kama Jeshi la Kujenga Uchumi tunafahamu wajibu wetu kwa wananchi na Serikali ndio maana tuliamua kuipatia Serikali jengo hili ili kudhibiti maradhi haya, tunafahamu kuwa maeneo ya jeshi hutumika kwa dharura za kiserikali hivyo tumetimiza wajibu wetu,” alisema Kanal Mussa.

Katika ziara hiyo Hamadi alikagua baadhi ya vituo vya afya katika ngazi za wilaya ambavyo vimeandaliwa kwa ajili ya kuvipa uwezo wa kutoa huduma ya mwanzo  kwa mtu mwenye dalili za corona.

 Alieleza kuwa wizara imeamua kuweka vituo 20 katika wilaya zote Unguja na Pemba ambapo 14 vipo Unguja na sita Pemba ili kurahisisha huduma katika kupambana na kudhiti ugonjwa huo.

Mkurugenzi wa Kinga Wizara ya Afya Zanzibar, Dk Fadhil Mohamed Abdallah, alisema lengo kuu la kuweka vituo hivyo wilayani ni kurahisisha na kupata uhakika wa taarifa za mtu mwenye dalili ili kupewa huduma ya uhakika.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles