31.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

ZAMBI: WATUMISHI WASIOSHIRIKI MAZOEZI WAPEWE BARUA ZA ONYO


Na Mwandishi wetu |

Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi amemuagiza Katibu Tawala wa Mkoa huo, Ramadhani Kaswa kuwaandikia barua ya onyo watumishi wote wa serikali na taasisi zake kwa kutoshiriki mazoezi.

Hatua hiyo inatokana na baadhi ya watumishi hao, kutoshiriki katika mazoezi ya kila Jumamosi ya pili ya mwezi ambayo ni utekelezaji wa agizo la Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan kwa Watanzania wote kushiriki mazoezi ya pamoja siku hiyo.

Zambi amesema hayo mwishoni mwa wiki hii katika Viwanja vya Ilulu, Manispaa ya Lindi yalikofanyika mazoezi hayo ambapo wananchi, watumishi wa serikali na vikundi mbalimbali vilishiriki.

Kwa mujibu wa Zambi, watumishi wasioshiriki katika mazoezi hayo ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Lindi, Ofisa Utumishi wa Halmashauri hiyo na Wakuu wa Idara, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Lindi, na Wakuu wake wa Idara Wa Halmashauri hiyo, Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Mkoa wa Lindi na watumishi wote wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Lindi.

“Mnajua hili zoezi baadhi ya watu wanalifanya kama utani, na tukifanya kama utani hatutafika na ni kwanini tunadhani ni lazima tubembelezane kwa manufaa ya kwako mwenyewe? Sasa kama mnataka niwabembeleze hiyo haitawezekena.

“Watumishi wote ambao hawajafika katika mazoezi leo waandikiwe barua za onyo ambayo itaandikwa barua ya onyo kwa kukaidi agizo la Makamu wa Rais, maana hiyo ndiyo itakuwa adhabu tosha kwao maana nimekuwa nikiwasisitiza mara kwa mara bila mafanikio sasa tukishaweka barua za onyo kwenye mafaili yao huenda watajifunza,” amesema Zambi

Zambi pia amemuagiza Katibu Tawala huyo kupeleka nakala za barua za watumishi hao pia kwa waziri anayehusika ili zibaki kama kumbukumbu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles