29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Zamalek, Casablanca kinawaka CAF leo

CAIRO, Misri

NI leo hiyo! Raja Casablanca watawaalika Zamalek katika Uwanja wa Mohamed V, ukiwa ni mtanange wa nusu fainali ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika, huku ule wa marudiano ukisubiriwa Oktoba 24, mwaka huu.

Hatua hiyo ya nusu ilianza jana kwa mechi nyingine ya kibabe kati ya wenyeji, Wydad Casablanca, na wageni wao kutoka Misri, Al Ahly.

Zamalek wanasaka ‘ndoo’ ya sita kwenye historia ya michuano hiyo, wakati Raja wao litakuwa taji lao la nne endapo watakuwa mabingwa msimu huu.

Ukiweka rekodi ubaoni, Zamalek wanaonekana kuwa ndiyo wababe kwani wameshinda mara mbili katika mechi nne dhidi ya Raja, huku wenzao hao wa Morocco wakitamba mara moja na kuambulia sare moja.

Ukame wa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa kwa timu zote mbili unaifanya mechi ya leo iwe ngumu. Zamalek watashuka dimbani wakiwa na kumbukumbu ya kulikosa taji hilo kwa miaka 18, wakati Raja wao hawajaliweka mkononi kwa miaka 20 sasa.

Kuelekea mchezo huo, Zamalek itawakosa mabeki Abdeljalil Jbira na Omar Boutayeb, kama itakavyokuwa kwa kiungo Abderrahim Achchakir, ambaye pia ni majeruhi.

Zamalek wao hawatakuwa na kiungo Shikabala, mabeki Mohamed Abdel Shafy na Hazem Imam, huku ‘mido’ wao raia wa Tunisia, Ferjani Sassi, naye akikosekana baada ya kugundulika kuwa na virusi vya Corona akiwa na timu ya taifa.

- Advertisement -

Related Articles

1 COMMENT

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles