29.1 C
Dar es Salaam
Thursday, December 8, 2022

Contact us: [email protected]

Zahivipunde| Wingi wa maji Mto Ruvu warejea zaidi ya wastani wa kawaida

*Wananchi kuondokana na mgawo wa maji

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Uwanda wa juu wa safu ya milima ya Uluguru, baadhi ya mito wingi wa maji umepanda leo Novemba 19, 2022 na maeneo mengine wingi wa maji umeendelea kupungua kidogo ukilinganisha na siku ya jana Novemba 18.

Hatua hiyo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa mapema leo Novemba 19, na mamlaka ya Bonde la Wami/Ruvu ambapo imeeleza kuwa dalili zinaonyesha kuwa bado kuna mvua zinatarajiwa kunyesha katika maeneo ya Safu ya Mlima Uluguru Wilaya ya Morogoro.

“Wingi wa maji ni kama ifuatavyo, Mto Ruvu eneo la Kibungo; lita 32,000 kwa sekunde. Kiasi hiki kiko juu ya wastani ukilinganisha na wastani wa muda mrefu (1950-2021) ambayo ni lita 18,000 kwa sekunde.

“Mto Mgeta eneo la Duthumi lita 8,150 kwa sekunde. Sawa na ongezeko la lita 1,550 kwa sekunde ukilinganisha na siku ya jana. Pia, Wingi wa Maji kwa siku ya leo uko juu ya wastani ukilinganisha na wastani wa muda mrefu (1950-2021) ambayo ni lita 5,521 kwa sekunde.

“Mto Mvuha eneo la Tulo lita 16,880 kwa sekunde. Wingi wa maji kwa siku ya leo uko juu ya wastani ukilinganisha na wastani wa muda mrefu (1950-2021). Mto Ngerengere eneo la Kongwa wingi wa maji ni lita 2,650 kwa sekunde,” imeeleza taarifa hiyo.

Aidha, imeongeza kuwa, uwanda wa Ruvu kati wingi wa maji umeendelea kuongezeka ambapo katika kituo cha Ruvu at Kidunda (1H3) wingi wa maji ni lita 15,870 kwa sekunde sawa na ongezeko la lita 3,280 kwa sekunde ukilingasha na siku ya jana

“Pia kwa uwanda wa Chini mto Ruvu ktk kituo cha 1H8A karibu na Mtambo wa DAWASA wa Ruvu juu, wingi wa maji umeongezeka na kufikia lita 9,203 kwa sekunde sawa na ongezeko la lita 731 kwa sekunde ukilinganisha na siku ya jana

“Aidha, wingi wa maji utaendelea kupanda zaidi ktk uwanda wa Ruvu chini kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha katika milima ya Uluguru ambayo ndyo chanzo cha Mto Ruvu,” imeeleza taarifa hiyo n kusisitiza kuwa taarifa ya hali ya maji itaendelea kutolewa kila wakati.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,692FollowersFollow
558,000SubscribersSubscribe

Latest Articles