29.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 1, 2023

Contact us: [email protected]

Zahera: Yanga hii mtaikoma

Theresia Gasper -Dar es salaam

KOCHA Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera, amesema timu yake itakuwa vizuri zaidi na kufanya kweli katika mchezo wa michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Township Rollers ya Botswana.

Yanga inatarajiwa kuwavaa Township Rollers kati ya Agosti ya 9 na 11 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kabla ya timu hizo kurudiana kati ya Agosti 23 na 25, mwaka huu, nchini Botswana.

Yanga juzi ilibanwa mbavu na Kariobang Sharks ya Kenya kwa sare ya bao 1-1 katika mchezo wa kirafiki uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya tamasha lao la Wiki ya Wananchi.

Akizungumza baada ya mchezo huo, Zahera alisema waliamua wasicheze mechi kubwa ya kirafiki katika kambi yao ili kuwafanyia ‘sapraizi’ mashabiki wao ya wachezaji wapya waliowasajili.

“Usajili ambao tumefanya msimu huu, niumeupenda kwani ukiangalia safu ya ushambuliaji kila mchezaji anapambana, anajua jinsi ya kutafuta mpira na kufunga, tofauti na msimu uliopita.

“Katika mchezo huu, wachezaji hawakuweza kucheza kwa kasi ile niliyoitaka kwa sababu katika mechi zote za kirafiki, tulicheza na timu ndogo, hali iliyowafanya wasiendane na kasi ya timu kubwa, lakini kwa siku hizi zilizobakia, watakuwa fiti zaidi na kufanya vizuri kwenye mchezo na Township Rollers,” alisema.

Alisema mshambuliaji wake, Sadney Urikhob, alikuwa haendani na kasi ya wenzake kwa sababu alichelewa kufika kambini, hivyo anatakiwa kufanya mazoezi zaidi ili awe fiti, lakini pia kupunguza kilo nne.

Zahera alisema kwa kikosi alichonacho, msimu ujao anaamini Yanga itatoa ushindani wa hali ya juu katika mechi zao.

“Tumecheza mechi hii na kesho kutwa (leo), tunatakiwa kusafiri kwenda Zanzibar kucheza tena na Mlandege Jumatano na Alhamisi tutacheza na Malindi FC, hapo naamini timu yetu itakuwa ipo tayari kwa ajili ya michuano ya kimataifa,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,404FollowersFollow
564,000SubscribersSubscribe

Latest Articles