24.6 C
Dar es Salaam
Monday, October 14, 2024

Contact us: [email protected]

Zahera kuikimbia Yanga msimu ujao

Lulu Ringo, Dar es Salaam

Kocha Mkuu wa Klabu ya Yanga, Mwinyi Zahera amesema msimu huu wa 2018/2019 ukimalizika ataachana na timu hiyo kutokana na washabiki, wanachama wa klabu hiyo kushindwa kujitolea kuisaidia timu yao.

Zahera ameiambia Mtanzania Digital kwamba anashangaa kuona Yanga ikijiita timu ya wananchi na yenye matajiri wengi lakini inashindwa kujisaidia yenyewe.

“Mimi nasema hivi ukijisaidia na Mungu anakusaidia, sasa mimi Kocha Zahera nimeamua Ligi hii ikimalizika naweza kuondoka Yanga sababu nimefanya mambo mengi sana kuisaidia timu lakini naona wanayanga wenyewe hawapendi kujisaidia.

“Kama nawaambia washabiki na wanachama tuijenge timu yetu sisi wenyewe na hakuna chochote kinachofanyika sitaweza kuendelea hivi,” amesema Zahera.

Mwanzoni mwa Februari mwaka huu Kocha Zahera alianzisha kampeni ya kuchangia klabu ya Yanga ambapo amesema pesa itakayopatika itatumika kununua wachezaji na kujenga uwanja wa mazoezi kwa msimu ujao.

Mratibu wa klabu ya Yanga, Hafidh Salehe Jana Februari 21, alitanga zaidi ya shilingi milioni 21 ndizo zilizopatika tangu kampeni hiyo kuanzishwa, kiasi kilichoonekana kutomridhisha Kocha Zahera kutokana na mipango mikubwa aliyo nayo baada ya msimu huu kuisha.

Zahera amesema anashangaa kuona wanachama na washabiki wa Yanga kuchangia kiasi hicho kwa takribani wiki nne toka kampeni hiyo ilipoanza.

“Hao matajiri wengi walioko Yanga kama kila wiki wanachangia Yanga pamoja na wanachama, mashabiki tunauwezo wa kupata fedha nyingi na mwezi wa tano tukanunua wachezaji wazuri na tukajenga uwanja wa mazoezi,” amesema Zahera.

“Kinachonishangaza zaidi mashabiki na wanachama wao wanalalamika tu timu inapofungwa, sasa nawaomba wajipange ni jinsi gani watayaepuka maumivu kila mara timu ikicheza wapende kujisaidia wenyewe.

“Basi nadhani Mungu hawezi kunilaumu kwa maamuzi ntakayochukua kwa kuamua kuachana na timu ya Yanga maana itakua vigumu sana kuendelea kujitolea wakati watu wao wenyewe hawapendi kujitolea,” amesema Kocha Zahera.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles