23.7 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

ZAHERA ATUA NA ‘SUMU’ YA PYRAMID

THERESIA GASPER-DAR ES SALAAM

KOCHA Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera, anatarajia kuungana na timu yake leo kuendelea na maandalizi ya mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Mbao FC na ule wa Kombe la Shirikisho Afrika watakapoivaa Pyramids ya Misri.

Zahera alikuwa nchini Cameroon pamoja na timu yake ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), ambapo walikuwa na mechi za kirafiki dhidi ya Algeria na Ivory Coast.

Yanga inakabiliwa na mchezo ya Ligi Kuu dhidi ya Mbao FC unaotarajiwa kuchezwa Oktoba 22, mwaka huu, Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

Lakini pia, kikosi hicho kina kibarua kigumu cha mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Pyramids unaotarajiwa kuchezwa Oktoba 27, mwaka huu katika dimba hilo CCM Kirumba.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano cha klabu hiyo, Hassan Bumbuli, alisema kikosi hicho kitaendelea na mazoezi leo kabla ya kwenda Mwanza Oktoba 20 mwaka huu kuivaa Mbao FC.

“Kwa sasa hatutacheza tena mchezo wa kirafiki baada ya jana (juzi) kuahirishwa ule wa Pan Africa kutokana na uwanja kujaa maji, hivyo kwa sasa tunaendelea na mazoezi ya kawaida,” alisema.

Alisema leo wachezaji wataendelea na mazoezi kama kawaida, huku akiweka wazi kuwa Zahera atakuwa ameshawasili kuendelea kukinoa kikosi hicho.

Bumbuli alisema mipango yao ni kwenda kupambana na kupata pointi tatu muhimu kwenye mchezo dhidi ya Mbao FC kabla ya kukutana na Pyramids.

Yanga itakutana na Mbao FC ikiwa imetoka kupata ushindi wa bao wa 1-0 dhidi ya Coastal Union katika mchezo uliochezwa Oktoba 5 mwaka huu, Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Katika msimamo wa Ligi Kuu Bara, Yanga inashika nafasi ya 14, ikijikusanyia pointi nne, sawa na Polisi Tanzania, Mbeya City, Coastal Union na KMC, timu hizo zikitofautiana kwa idadi ya mabao ya kufunga na kufungwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles