23 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

ZAHERA APIGA BAO TFF

THERESIA GASPER-DAR ES SALAAM

KILIO cha Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera kuomba mechi zao zisogezwe mbele ili kutoa nafasi kwa wachezaji wake kupata muda wa kumpumzika, hatimaye kimesikilizwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).

Yanga ilipangwa kucheza na Polisi Tanzania kesho kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Lakini kwa kuwa kikosi hicho kilikuwa nchini Zambia kwa ajili ya mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Zesco, Yanga waliomba TFF kusogeza mbele kipute chao dhidi ya Polisi Tanzania.

Wanajangwani hao walituma ombi lao hilo TFF kwa kuwa wasingepata muda wa kupumzika baada ya kutua nchini wakitokea Zambia, kwani fungu la kwanza la msafara wao lilitarajiwa kuwasili jana usiku, wakati lingine ni leo alfajiri, ikiwa ni saa chache kabla ya mchezo wao wa kesho.

Hatimaye TFF imekubali mchezo huo kuchezwa keshokutwa Alhamisi na si kesho.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano Yanga, Hassan Bumbuli, alisema walituma barua TFF ya maombi ya kusogezwa mbele kwa mechi hiyo kutokana na wachezaji wao kuchelewa kurejea.

Juu ya ombi lao hilo, Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Ligi, Boniface Wambura, aliliambia MTANZANIA jana akisema: “Tumesogeza mbele mechi ya Yanga na Polisi Tanzania ambako itachezwa siku ya Alhamisi ili wapate muda wa kujiandaa baada ya kuwasili.”

Kwa uamuzi huo wa TFF, ni wazi Zahera atapata muda wa kuwaandaa vijana wake kwa mchezo huo na hivyo kutokuwa na kisingizio cha kutozoa pointi zote tatu.

Katika mchezo wao dhidi ya Zesco United, Yanga ilifungwa mabao 2-1 na hivyo kutolewa kwenye michuano hiyo ya Afrika kwa kipigo cha jumla cha mabao 3-2, baada ya sare ya bao 1-1 walipokutana kwa mara ya kwanza jijini Dar es Salaam.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles